Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Ila wadau tuacheni masikhara haya mambo ya kazi yana usiri sana ndan yake yan haiwezekan hii jf ikakosa Watu ambao walifanya Oral MUCE na wakapigiwa simu na kuripoti kazini lakin nao uzi Wetu wanauona bt hata kututonya kuwa tumepigiwa simu na Watu tushaenda kituo cha kazi.
 
Unajua nilichojifunza humu jf watu Wana roho mbaya sana mkuu ,Yani unaweza kukuta mtu anajua kitu lakini hata kumuelekeza mtu hataki
 
Wapo ila ile kasumba ya ukishapata unasahau na wengine ndiyo inayowasibu.
 
Unajua nilichojifunza humu jf watu Wana roho mbaya sana mkuu ,Yani unaweza kukuta mtu anajua kitu lakini hata kumuelekeza mtu hataki
Kila mwaka watu wanapiga mikando Utumishi ila kutoa muongozo humu hakuna.

Jana nilikuwa naperuzi placements za mwaka 2020, nikakuta wapo wanalamba Asali NAOT(watu wa CPA na ICT) tangu August mwaka huo, na placement yao haikucheleweshwa sana(written ilikuwa May, placement June, kazini August) huenda PSRS ilikuwa haijatingwa kama sasa.

Pamoja na ofisi hiyo kuwa busy ila hatujawahi kusikia miongozo ya mikando kutoka kwa watu kama hao waliopitia mikando.

Japo watu wanaweza wakawa busy pia na mambo ya kukuza uchumi binafsi ila hilo haliwezi kuniaminisha kuwa hawapo humu JF.

Chonde chonde tukipata asali kupitia humu, tuendelee kutoa miongozo kwa wengine.
 
Mambo yanaenda yakubadirika, na hata namna usahili unavoendeshwa na maswali yanavyokuja hubadilika badilika sana, tusiwe na mtazamo "negative" sana.

Kuna miaka ilikua ukiingia katika usahil kukutana na maswali ya research ni kawaida, naona mwaka huu imekua sivyo, wanasema kila usahili ni "experience mpya".

Kuna mdau alishawahi pandisha uzi akijaribu kujenga hoja kuwa namna sahili zinavyoendeshwa sasa, zinawabeba sana fresh from collages/universities kwa kuwa paper zinabase sana katika videsa. Kwa maana hiyo huwawia vigum wenye uzoefu mda mrefu kazini na waliomaliza shule kitambo kushindana katika pace sawa na freshers.

Na tukumbuke pia wengine huamini kuwa, "Mafanikio ni siri, na siri ndio mafanikio".
 
Kwa hiyo tuseme hata idadi ya maswali, muda wa kufanya, kujibu short and clear napo panabadilika? hizi information ni muhimu, wengi wetu tuliokuwa hatujawahi kufanya tulipoenda tukajikuta tunaandika ma essay na tukachezea za kichwa, laiti tungepata muongozo wa kuwa unatakiwa uende direct kwenye point ingekuwa poa sana.

Hata kama mambo yanabadilika kuna baadhi hayabadiliki, na haya ndio tunapaswa kujuza wengine
 
Kabisa, kuna raia hizo hizo post za NAOT walishiriki mwaka 2020, na mwaka huu pia lakini si ajabu zote mtu akashindwa kuingia hata oral.

Hubadilika sana, jamaa wa HESLB hapo juzi wameshuhudia, zile roles wameambiwa wataje tatu na kuelezea mifano yake, ni mode mpya kabisaa. Watu walishazoea kuambiwa wa-mention tu hizo role, wakawa wanashuka kama zilivyoelezwa katika tangazo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…