Maandalizi ya Bajeti ya Mishahara: Maandalizi ya bajeti ya mishahara
yamekuwa yakizingatia miongozo na nyaraka mbalimbali zinazotolewa na Ofisi ya
Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora (OR – MUUB) na
Wizara ya Fedha na Mipango. Pamoja na maandalizi hayo, kumekuwa na
changamoto ya mahitaji makubwa ya masuala ya mishahara ikilinganishwa na bajeti
halisi inayoidhinishwa
1.6.
Maandalizi ya Bajeti ya Mishahara
92.
Wakati wa kuandaa ikama na bajeti ya mishahara kwa Mwaka 2023/24,
Maafisa Masuuli wanaelekezwa yafuatayo:
(i)
Kutoajiri watumishi wapya hadi kuthibitisha upungufu uliopo na iwapo
kuna waliozidi wahamishiwe sehemu zenye upungufu ili kuhakikisha uwepo
wa msawazo wa watumishi (Manning Level);
(ii)
Kutenga bajeti ya upandishaji vyeo, ajira mpya, ubadilishaji kada/kazi, nafasi
za kuhamia na uteuzi kwa kuzingatia Mwongozo wa Katibu Mkuu (ORMUUB) kuhusu uandaaji wa ikama na makadirio ya bajeti ya mishahara kwa
Mwaka 2023/24;
(iii)
Kujumuisha nyongeza ya mwaka ya mishahara (annual increment) katika
bajeti ya mishahara kwa mwaka 2023/24 kulingana na ukomo wa bajeti
uliopo;
(iv)
Kuhakikisha kila mtumishi anachangiwa katika Mfuko wa Pensheni na
Hifadhi ya Jamii kwa kiwango sahihi kinachotakiwa kwa mujibu wa sheria ili
kuepuka tozo inayotakana na ucheleweshaji wa mchango.