Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

MWALIKO WA KUPOKEA MAONI YA ONLINE APTITUDE TEST

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Hassan O. Kitenge amekuwa akisikiliza na kutatua changamoto mbalimbali za wadau katika Suala zima la Ajira. Hivyo, ili kupata suluhisho la kudumu, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma imeanza mchakato wa kujenga mfumo wa kieletroniki ambao utawawezesha waombaji wa fursa za ajira kufanya usaili wa kuandika kwenye ngazi za Mikoa na Wilaya kupitia vituo maalum.

Ili kufanikisha zoezi hilo, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inatarajia kukusanya maoni na mahitaji ya mfumo huu kutoka kwa wadau wake, hususan waombaji kazi katika vituo vya Dodoma na Dar es Salaam katika kumbi ambazo mtajulishwa. Vikao hivi vya wadau vitafanyika kuanzia tarehe 09 -12 Januari 2023. Kwa kituo cha Dodoma, kikao cha wadau kitafanyika tarehe 9 Januari, 2022 na Dar es Salaam kitafanyika tarehe 11-12 Januari, 2022.

******************

Wakuu nendeni mkatoe maoni, kwa mtazamo wangu naona hii itasaidia sana kupunguza jam la written halafu pia kila mtu atakaeomba atapata nafasi ya kujitetea.

Source: PSRS website
 
ngoja nitume maoni yangu na mm

Sent from my Redmi 5 Plus using JamiiForums mobile app
 
Me naona ilikuwa hamna haja ya hadi kukutana huko.Maoni yote yapo kwenye huu uzi,waufuatilie tu.


Saili zifanyike katika mikoa na oral ndo ikafanyike Asha Rose Migiro kule
 

Mkuu asante sana, na upande wa pili kwa wale wenye elimu za taaluma tofauti hasa ambazo sio za ngazi za elimu.


Kwa mfano mtu ana degree yake ya uhasibu ila amesoma na kupata certification ya masuala ya bima ambayo ni nyeti sana kwa wanaosoma mambo hayo.

Au unakuta mtu ana shahada ya business admin ila akasoma certification ya bodi ya masuala ya ugavi.

Hawa watu wanafanyaje ili wawe na urahisi wa kuomba kazi za taaluma zote?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…