MWALIKO WA KUPOKEA MAONI YA ONLINE APTITUDE TEST
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Hassan O. Kitenge amekuwa akisikiliza na kutatua changamoto mbalimbali za wadau katika Suala zima la Ajira. Hivyo, ili kupata suluhisho la kudumu, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma imeanza mchakato wa kujenga mfumo wa kieletroniki ambao utawawezesha waombaji wa fursa za ajira kufanya usaili wa kuandika kwenye ngazi za Mikoa na Wilaya kupitia vituo maalum.
Ili kufanikisha zoezi hilo, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inatarajia kukusanya maoni na mahitaji ya mfumo huu kutoka kwa wadau wake, hususan waombaji kazi katika vituo vya Dodoma na Dar es Salaam katika kumbi ambazo mtajulishwa. Vikao hivi vya wadau vitafanyika kuanzia tarehe 09 -12 Januari 2023. Kwa kituo cha Dodoma, kikao cha wadau kitafanyika tarehe 9 Januari, 2022 na Dar es Salaam kitafanyika tarehe 11-12 Januari, 2022.
******************
Wakuu nendeni mkatoe maoni, kwa mtazamo wangu naona hii itasaidia sana kupunguza jam la written halafu pia kila mtu atakaeomba atapata nafasi ya kujitetea.
Source: PSRS website