Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Niliona kwenye mkataba wa utendaji kazi wa PSRS na wateja wake kuwa tangazo likipelekwa kwao watalifanyia kazi(kulitangaza) ndani ya siku 14.

Kuchambua maombi ni kwa mwezi 1 tangu deadline iishe.

Ila kutokana na nyomi kubwa huo muda unakuwa hautoshi ndio maana shortlists zinatoka baada ya muda mrefu sana
 
Wakuu ndo nimepanda gari kurudi dar huko utumishi na kureport kazini process kubwa sana kichwa kinauma hapa aiseee ngoja nisinzie tu hapa kwenye kiti
Pole sana mkuu, nilijua hili la process ila sikulisema nilitaka wahusika mje mliseme.

Unakumbuka placement ya mwisho ilitoka tarehe 19/7/2022?(ukiachana na placements za vyuo na Bunge)

Sasa kuna jamaa namfahamu alipangiwa kituo katika hiyo placement, alipoenda kuchukua barua PSRS akatakiwa aipeleke kwa mwajiri, alipoenda kwa mwajiri akaambiwa asubiri mchakato wa ajira uchakatwe na atajulishwa(kupangiwa kituo).

Juzi wakati placement yenu inatoka ndio jamaa kapokea barua yake ya kazi kutoka kwa mwajiri ambayo ataenda nayo kuripoti kwa Manager wa kanda ili akapangiwe majukumu.

Yaani miezi 2 imekata ndio anaenda kuanza kazi sasahivi.

Sasa wewe omba mchakato usiwe mrefu la sivyo utaanza kazi Novemba huko.
 
Kwanini inakuwa hivi mkuu kwani kuna process gani wanafanya baada yakupeleka barua kutoka utumishi?
 

Hili ni sahihi sana, ni wazi wameshindwa kutekeleza ahadi walizoahidi wateja wao.
 

Noma mkuu mwezi huu na miwili inayokuja inaweza kuisha kabisa bila shida na Bado tukawa mtaani tu duh process kubwa sana Yan ndo kwanza una lipoti makao makuu then wachakate ndo upangiwe kituo cha kazi dah😂🤣 mie interview ikijaa naenda kudadeki na placement nyingine ikitoka sijui itakuaje aiseee

Copy kibao za vyeti wanataka mia kasoro, mara hostiptal check up, nida copy,bank copy hahaahahahahhaa nimeenda kufanya check up Sina ugojwa namaliza process zote

Nishapata ugojwa wa ulemavu wa miguu nimetembea mpka nimekoma
 
Wakuu nipeni mbinu ya kusoma ili nipambane vema hizi saili za UTUMISHI, maana nilisoma kitambo na material s yashaanza kupotea. Ninyi mnatumia mbinu gani
Unapofanya application anza kusoma siku hiyo mpk pale mtakapoitwa, hakikisha kila siku unaingiza kitu kipya na kujikumbusha ya nyuma!

Tafuta maswali mbalimbali mtandaoni.

Jiandae na Practical ila inahitaji uzoefu kdg.

Wahi mapema kwny interview

Hakikisha unajibu maswali mawili kwa uhakika na mengine ukiweza

Ukizingatia hayo naamini utatoboa mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…