Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Karibuni katika mkando wa kesho wasaka mirija ya Asali.

Mkija kutusindikiza na Ngoma ya Mkando Ft official tutapata mzuka wa kukabili mkando ipasanyo[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
We jamaa unapenda kupeana moyo kwenye hamna [emoji16][emoji16].. hata kama Hali ni Tete,, hv huoni hyo Mikandamizo kutoka PSRS kwa vijna wenzio..?

Hahaha, ni kweli Mkuu, wakati huu ambapo vijana tunapigania maisha ndio muda mzuri wa kupeana mitazamo chanya, na tunaihitaji zaidi ili kupiga hatua, mwisho wa siku hizi nyakati zinapita na zitabaki simulizi Mkuu.
 
Duh ! Maana Sisi wahandisi hizo sahili zenyewe za kuhesabu , yaani kweli kweli utakuta kazi nafasi 1 watu shortlisted zaidi ya mia tatu .
Bora WA biashara kidogo naona wanakuwa na mikeka mirefu mfano TRA Ila uhandisi nchi hii ni majanga
Hii nchi ya ovyo Sana ,wahandisi wamesahaulika kabisa .

Ni kweli kabisa Mkuu, na mambo naona yameenda kinyume sana, miaka ya nyuma kidogo ilikuwa watu wa Sayansi kiujumla mkimaliza tu masomo hamcheleweshwi, mnaingia kazini ila watu wa sanaa na biashara ilikuwa ni lazima usote vya kutosha, lakini naona kwa sasa imekuwa kinyume chake.
 
Back
Top Bottom