Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Hahaha, Mkuu una michezo ya hatari sana.

Ndugu wasaka ajira naomba nirudie mara kwa mara hii kauli mpaka inase vichwani hadi tunakufa, na ikiwezekana kila tukiamka asubuhi tuiseme mara sita na tusukumie na glass ya maji baridi, ni hivi: “KWA SOKO LA AJIRA LA TANZANIA KWA SASA, KUPATA KUNA MAANA ZAIDI KULIKO UMEPATA NINI”.

Mimi naamini mpaka mtu uliiomba nafasi, kuna mazuri uliyaforesee kwenye hiyo taasisi.

Kuliweka ombi lako la ushauri kwa lugha rahisi ni kwamba, unataka uachane na ajira uliyoipata ili ukatafute ambayo ni bora zaidi ila bado hujaipata na huna uhakika wa kuipata, Hahaha.

Anza kwa kujiuliza tofauti na hiyo ajira uliyoipata sasa hivi una ajira ipi, ili hata ukikosa zote hii ya NGO na NAOT ujue utabaki na kipi, kama huna au iliyopo ni mbovu zaidi akili ikucheze, kama unayo ya maana zaidi, hakuna shida fanya maamuzi yoyote hutakuwa umekosea.

Mkuu angalia uwezekano wa kwenda sehemu zote mbili, ikishindikana nenda ulikopata.
UMEMALIZA MKUU👏👏👏👏
 
Naombeni ushauri wadau leo nimepigiwa simu ya kuripoti kazini private non profit org salary 1.4m na kesho natakiwa niende dom kupiga usaili naot nafas 3 nifanyeje akili imestuck
Mkuu ivi unaachaje kwenda kukamilisha dili la 1.4M kisa usaili ambao probability ya kupata ni ndogo sana kutokana na competition.

Hizi saili za NAOT na HESLB sio saili za mwisho mkuu.

Nenda kavute mpunga kwanza ili ukiwa unaadhurulia saili nyingine unakua comfortable.
 
Bajeti ya nauli tuinywee supu hapo saba saba basi
Nimepata chimbo langu la bei rahisi huku nzuguni.bei ya room per day ni elfu 8,maji yapo,na chumba ni kizuri tu.mtaani chai kikombe ni 200/=,andazi 200/= chapati ni 300/=.supu inaanzia 1000/=,ugali dagaa ni kuna wa 1000/= na wa 1,500/=.
Naamini nimepunguza cost mno tofauti na ningekaa maeneo ya town huko.
 
Huoni utapata gharama yakusafiri asubuhi kwenda udom???maana hapo watakupiga buku 8 mpaka 10 kwa boda
 
Huoni utapata gharama yakusafiri asubuhi kwenda udom???maana hapo watakupiga buku 8 mpaka 10 kwa boda
Uzuri usaili mpaka wamalize kukagua vyeti ni saa 3,so nikiamka saa 12 asubuhi nikachukua daladala mpaka sabasaba then nikachukua ya udom..naamini saa 1 na dakika kadhaa ntakua udom .
Uzuri tushakua wazoefu wa hizi mambo,so hakuna kujitesa sana kama ilivyokua mwanzo.
 
Nimepata chimbo langu la bei rahisi huku nzuguni.bei ya room per day ni elfu 8,maji yapo,na chumba ni kizuri tu.mtaani chai kikombe ni 200/=,andazi 200/= chapati ni 300/=.supu inaanzia 1000/=,ugali dagaa ni kuna wa 1000/= na wa 1,500/=.
Naamini nimepunguza cost mno tofauti na ningekaa maeneo ya town huko.
Hilo chimbo limelielewa aisee
 
Back
Top Bottom