Basi tuishi kwenye subira ya PDF tutajua mbivu na mbichi.
Ila nikiwa heki jamaa zangu waliowengi washapika hatua aisee.
Ninapoishi kuna kiwanda karibu cha kutengeneza dawa za mifugo, miaka kadhaa imepita kumbe jamaa yangu(class mate) anapiga kazi pale na kashakuwa promoted kawa Manager wa Quality Control,
Kuna siku mida ya saa moja asubuhi nikiwa kwenye harakati za kuelekea kijiweni natembea barabarani, IST ikaja kutoka nyuma, nikasogea kuipisha ilipokaribia ikasimama na kioo kushushwa chini, nikasikia sauti nilipoangalia nikakuta ni classmate.
Nikamsogelea kumpa hai nikamuuliza anakoelekea akaniambia anaenda pale kiwandani, nikamsindikiza kwa kunipa lift maana mwenyewe nilikuwa napitia pale kiwandani niende kijiweni.
Kwenye kumuuliza kaanza lini kazi, kaniambia ameanza miaka kadhaa nyuma, mimi nikabaki kujikaza kujielezea jinsi ninavyopigika kijiweni ili angalau nionekane nipo kwenye game[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3], huku moyoni nikigubikwa na unyonge wa kujiuliza "nakwama wapi"
Wengine tupo kama mabeki kwenye mpira ambao kufunga goli unaweza ufunge moja tu msimu mzima, huku wengine wakijinyakulia Golden shoe