Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Shida inaweza kuwa jinsi anavyojibu maswali au anaweza kuwa alilielewa swali vibaya
Kwamfano unaweza ulizwa
Describe land forms of geomophic process
Au Describe features due to geomophic process
Hayo maswali ukiyaangalia ni kama yanafanana lakini yapo tofauti kwahiyo kwenye zile pepa ukiyumba kulielewa swali yani ujue marks 25 zote hazipo tena

Duh! Sawa mkuu, kwa usawa huu itabidi bajeti ya kufanya usaili ibaki ya kwenda Dodoma mara moja, zoezi liendelee mwakani Mungu akipenda, hata kama akiitwa zaidi ya mara moja, nitamwambia aangalie anayoamini ana uhakika zaidi.

Ndugu zangu hizi gharama za nenda rudi Dodoma sio za mchezo.
 
Hizi paper mara nyingi zinahitaji mambo makuu kama matano.

1. Kuelewa maswali
2. Kuandika kwa kifupi, usiweke mambo mengi sana.
3. Speed ya kuandika iwe kubwa, maana dakika 40 ni chache sana ukishaingia mule. Andika kwa speed ya jet. Watu huwa hawamalizi maswali kwa kuandika polepole.
4. Maandalizi kabla ya paper. Jiandae na usome vizuri.
5. Kama unaamini ktk Mungu, omba.

Nimeupokea ushauri Mkuu, na nitamuweka sawa dogo.
 
Kuwa na faraja sana, nilikuwa na vikao na maafisa wa Utumishi leo, ikiwezekana hizi saili usifanye sio Written wala Oral, nataka jina lako lionekane moja kwa moja kwenye pdf ya placement.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Aisee tuwaombee wadogo zetu na majobless wote wapate mrija wa asali...mimi mdogo wangu tangu 2019 anafanyaga interview ila ndio hivyo bahati haiwi upande wake ....namuonea huruma na kama familia tunamsapot ....ngoja tusubiri maana juzi kati kafanya interview hizi za LGA NA MDA kama auditor amefanya oral na nilikuja kumuulizia hints humu za kujibu oral nashukuru wadau walinijibu nikampa nondo hope this time mambo yatakuwa mazuri upande wake ...nitaleta mrejesho

Aisee kupitia hili la kwako nafarijika sana, nilifikiria nalipitia peke yangu. Kuna muda huwa ananiambia anahisi kama anaonekana ni kilaza, kitu ambacho kinamuumiza sana.

Madogo wakikwama kwenye hizi saili huwa wanadhani wanaumia peke yao, kumbe hata wanaotutegemea huwa tunaumia kwa kuvaa viatu vyao sometimes.

Ngoja niendelee kumjenga kifikra, naamini siku yake ipo.
 
Back
Top Bottom