Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

@wizy kama ameamua kukimbia jukwaa ama kwa kukanda au kukandwa atatutia aibu wanaume tunaopaswa kupambana hadi tone la mwisho jasho.

Tuendelee kumsubiri huenda akaja, asipokuja au aje na utambulisho mpya napo sio mbaya, wengine tuendelee na harakati za kuusaka mrija wa Asali kama kawaida
jaman pengine hata bando limekata,mpeni muda tu
 
Lakini status yake si alisema inasoma SELECTED FOR NULL
Mi nahisi wote mliofanya inasoma ivyo au iwe wote mlioandikiwa selected for null mumepita oral wakafanya vetting kulingana na nafasi labda mtu 1 akachukuliwa kulingana na ufinyu wa nafasi wengine mtakaa database make kuna yenye selected for null green na not selected for null red sasa unaweza kuta kada mumefaulu wote watafanyaje
 
Zamani veta ukimaliza level 2 kwenda 3 Lazima urudishe cheti cha level 2 ikatokea nafasi ya level 2 nkaomba cheti cha level tu sina ila na barua ya mkuu wa kanda inayoonyesha namba ya cheti changu cha level 2 kufika usaili oral nikazuiwa baadae nikaruhusiwa je hapo utakuta wameniridhisha tu ionekane nimefanya tayari ni mkando au ile barua naweza fanikisha
 
Msaada
Kwa mzoefu wa safari za Arusha-Dom wapi naweza pata private ijumaa kuanzia saa 11 jioni.
Mkuu nenda majengo chini kule karibu na Aim mall.Kuna jamaa pale wanakusimamishia kuuliza gari zote,japo kwa muda huo ni changamoto waweza kosa.

Me nimewahi sota hapo kuanzia saa kumi mpaka saa moja na nusu ndo nikapata lori na safari ni usiku very risk
 
Kwa nature ya humu Ndani.. inaonesha vijana tuna presha sana kwenye kusubiria placements kuliko presha ya kwenye interviews, written and Oral.
Wale watu wa karibu na wizy tuambieni Huyu jamaa Yuko wapi Sasa maana kimya sana na alikuwa anafurahisha genge hapa.
 
Mimi nina imani kila mmoja akiweka jitihada katika dhamira zake atafanikiwa kwa wakati wake ambao mungu amepanga kukosa au kupata kuna kusudio kubwa wala hatupaswi kuvunjika moyo,,,Wale mnaoenda kwe usaili wa awali simamieni ndoto zenu kwa makini na mjibu maswali clear pasi kuweka mbwembwe nyingi hawa watu hawana muda wa kusoma mambo mengi na kingine tumtangulize mungu katika kila hatua kwani ni muweza wa yoote
 
Uzi umepooza na kila mtu kushikwa na butwaa kihusu mwenzetu Wizy kutikuja amepatwa na nini kama ni kukosa mrija hilo ni jambo la kawaida na huenda mungu amempangia sehemu njema zaidi ya ile,,,huko uliko wizy kama umefanikiwa hongera kama hakuna basi tunaamini siyo mwisho wa mapambano
 
Kwa nature ya humu Ndani.. inaonesha vijana tuna presha sana kwenye kusubiria placements kuliko presha ya kwenye interviews, written and Oral.
Wale watu wa karibu na wizy tuambieni Huyu jamaa Yuko wapi Sasa maana kimya sana na alikuwa anafurahisha genge hapa.
Wizy alivuta attention ya wengi kwenye huu Uzi hvyo tulitamani kujua matokeo yake kama mazuri tusherekee pamoja kama sio mazuri pia tufarijiane pamoja,ila pia nadhani tumuache ana haki ya uhuru wake binafsi tumpe muda akiona inafaa ataungana nasi
 
Back
Top Bottom