@wizy popote ulipo tunakuomba urudi.
Riziki ipo, kila mmoja wetu amekadiriwa riziki yake na muumba wake na hauwezi kuondoka juu ya mgongo wa ardhi kabla haujaichakata riziki yako.
Mtihani tulioachiwa ni njia za namna ya kuichuma hiyo riziki na kila mmoja atatumia njia yeyote ile ili aweze kuchuma riziki yake.
Wengi wetu kwenye uzi tumeona njia bora ya kuiendea riziki ni kupambana na PSRS ingawa kuna njia lukuki ambazo tunaweza kupita nazo na tukafanikiwa.
Katika hizi njia kuna mabonde, miinuko, tambarare, visiki, matope, utelezi[emoji3][emoji3](sio ule lakini) ambavyo vinafanya pawe na changamoto mbalimbali tunazopaswa kuzikabili ili tuweze kupita.
Mtu unakandwa mara kadhaa, hapo umekumbana na miinuko, matope, visiki. Ili uweze kupita lazima ukae chini ubuni mbinu za kuzitumia mwishowe unapita (unafika oral)
Mwingine anapitia njia ya utelezi/mserereko(written 1 tu kawakanda, oral 1 tu kawakanda).
Tunapitishwa katika hizo njia zote na mgawa riziki huku akiwa na maana yake yeye pekee(kama maana ya mabadiliko ya status baada ya oral kutokana na programming kama anavyosemaga
wizy ).
Hivyo basi tunapaswa kushukuru kwa jambo lolote lile maana kila jambo hutokea likiwa na sababu yake kwani unaweza kulalamika kuhusu kitu fulani kumbe umeepushwa na shari.
Tuwe na subira, tumtangulize Muumba/mgawa riziki.