Ni sahihi hujanielewa. Ila maelezo yako ni sahihi hata mimi vyeti vya shule, chuo, usajili vyote vina majina 2 ila cha kuzaliwa na NIDA ni majina 3. Na sijawahi kusumbuliwa popote.
Sasa maelezo yangu yalikuwa hivi nilipokuwa namhoji huyo jamaa:
Yeye amedai kuwa cheti cha chuo kinasomeka hivi: SAMIA SULUHU HANGAYA. Ambapo ni sawa na NIDA na kuzaliwa.
Halafu vyeti vya shule(form 4 na 6) vinasomeka hivi: SAMIA S HANGAYA, je umeona utofauti?
Sasa mimi nikahoji hivi:
Ukiwa unafanyiwa Admission chuo huwa wanatumia vyeti vya shule form 4 na 6(hapa mara nyingi wanatumia namba ya mtihani maana vyeti vinakuwa bado havijakamilika), kwa mantiki hiyo jina kwenye cheti cha chuo lazima lifanane na la kwenye vyeti vya shule(form 4 na 6).
Sasa huyo jamaa, vyeti vya shule na chuo vina utofauti wa majina kama nilivyotolea mfano hapo juu.
Ndio nikahoji kuwa, ilikuwaje chuo watumie jina la NIDA na kuzaliwa badala la kwenye vyeti vya shule ambapo taarifa zake zipo NECTA maana ukisearch namba ya mtihani inakuletea jina kamili.
Sijui umenielewa?