JMF
JF-Expert Member
- Jun 29, 2013
- 1,758
- 2,770
Mimi mwaka 2020 niliwahi kuwa SELECTED for oral interview na siku ya usahili nikasafiri toka Arusha kwenda Dar kwaajili ya interview jina likakosekana kwenye orodha ya wasahiliwa. Walinikataa na kudai wao wanafuata orodha waliyopokea toka watu wa database.Waheshimiwa, mimi na rafiki yangu tumekuja utumishi kuchukua barua zetu za kuitwa kazini.
Rafiki yangu amepata,
Na jamaa mwingine pia amepata.
Ila mimi wananiambia barua yangu hawaioni hivyo niache mawasiliano yangu kisha watanipigia ikishakuwa tayari ili nisafiri tena kutoka mkoa ninaoishi kuja Dodoma kuifuata.
Hii imekaaje wakuu, yaani barua za wengine zipo ila yangu haipo wakati sote tumepata kazi taasisi moja??
Ushauri wenu wadau.
Sent from my TECNO LC6a using JamiiForums mobile app