Kuna kanzidata za aina tatu:
1. Za wahitimu wa Vyuo na Wataalam
2. Za waliofaulu usaili
3. Za waliopangiwa vituo vya kazi.
Najikita kwenye Kanzi data ya waliofaulu usaili ambayo imezungumziwa kwenye kanuni namba 22.
Imelezewa kuwa orodha ya waliofaulu usahili mahojiano na hawakuweza kupata nafasi itatunzwa kwa matumizi ya baadae(1), itatumika kujaza nafasi wazi kulingana na mahitaji ya waajiri(2), endapo hii orodha itakuwa imeisha baada ya watu wote kupangiwa vituo vya kazi au waliopo kanzi data watakuwa hawana sifa au utaalamu anaouhitaji mwajiri, nafasi za ajira zitatangazwa(3),
Kulingana na hivyo vipengele vya kanuni inaonesha kuwa sifa au utaalamu wa mtu aliyepo kanzi data ndio utamuwezesha kupangiwa kituo endapo nafasi yenye kuhitaji sifa au utaalamu alionao itapatikana, hapa sasa ndio pale tunapoona watu wanapangiwa vituo kwenye taasisi tofauti tofauti ambazo hawakuzifanyia usahili.
Kuhusu kuangalia suala la qualifications za vyeti kama unavyotaka hapa mimi naona hili lipo ndani ya sifa au utaalamu uliotajwa kwenye kanuni hii.