Nilianza harakati hizi za kuusaka mrija nikiwa nikichangia kwenye nyuzi za jukwaa hili na ID yangu hii, sifikirii mwisho wangu uje uwe hivyo.
Mara nyingi watu humu JF walikuwa wanajua kuwa mimi ni mlamba Asali isipokuwa wachache wanaonifahamu/tunaofahamiana nje na JF, kama ningetaka watu waendelee kufahamu hivyo nisingekuwa nashiriki kwenye hizi nyuzi kwa ID hii, ningefungua ID nyingine wasioifahamu watu.
Humu kwenye uzi huu, yupo anayenifahamu ingawa hajawahi kukutana na mimi.
Kwa hiyo nikipata hiyo nafasi NAOT nitaleta mrejesho humu, tutafurahia wote humu hatua hiyo muhimu ya kuungwa kwenye gridi ya Taifa ya walamba Asali, watakaoweza kunifahamu nina imani watakuwa wachache miongoni mwa wengi tuliomo JF.