Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Hongera sana kaka, hakika tumefurahi aisee... Umetupa moyo wengi hatimae na wewe unaenda kulamba asali hakika ni furaha ilioje
Ahsante sana mkuu, Mungu ni mwema sana anatufanya tulambe asali mmoja baada ya mwingine
 
Jamaa Obviously ametumotevate sana vijana wenzie humu kwa kiasi kikubwa kwa madini Mbalimbali. Uungwana alikuwanao pia umefanya watu waapreciate mafanikio aliyoyapata.
Pia kitu ambacho niliona ni Cha kitofauti sana kwa jamaa tofauti na wengi wetu tuliopo humu kuwa jamaa alikuwa muwazi sana, kashakandwa saili kibao Ila hakusita kuleta mrejesho humu hii ilionesha kuwa jamaa ana ukomavu wa hali ya juu sana na hii ilipelekea baadhi ya watu hata kumwonea huruma na kumwombea japo kwa saili moja hii aliyofanikiwa kuingia Oral basi Mungu amtendee miujiza na kweli Mungu katenda.

Bila kusahau kuwa Mwifwa hana wivu licha ya yeye kukandwa na kupoteza mafanikio ya kupata kazi bado alizidi kuwapongeza wale waliokuwa wanafanikiwa na kuwatakia majukumu mema..

Hii iko poa sana, Mungu atutendee miujiza wote humu kwenye hii safari yetu tufike salam
Ahsante sana mkuu, tuishi kwa wema wakati wote
 
Mimi toka jana naugulia maumivu ya kukandwa nikashindwa hata kuwapongeza waliopata......sijaamini bado kuwa nimekosa nafasi zile za NPS. Ha ha ha. Written nilifanya fresh kabisa, na huko oral sijui nini kilibadilika...

Anyway ndiyo life hilo...maisha lazima yaendelee. Hongereni mliopata mrija wa asali. Jina la Mungu lipewe sifa.
Pole sana mkuu, Be strong, haikuwa riziki yako, riziki yako ipo muda ukifika hamna wa kuizuia.

Tuendelee kupambana
 
Uliwahi kusikia ripoti ya CAG ambapo wanaume walionekana kupata huduma ya kujifungua kwa Bima ya Afya?[emoji3][emoji3][emoji3]

Kwa hiyo accountant anaweza kubaini hili?
Watu Wengi wanajua Auditing ni Accounting and finance, Auditing ni kitu kipana Sana, na Kuna Auditing ambazo ziko very specific eg Pharmacy, Medical, Water resources,Ujenzi, ndio maana unakuta NAOT Kuna engineers,MD,Teachers, Pharmacists, Quantity Surveyors
 
Hongera sana Mkuu, we ni mtu humble sana.

Mimi nimekufahamu hata kabla ya huu Uzi, siku zote hujawahi badilika.
MUNGU akutangulie katika Utumishi mwema.
Na aibariki Familia yako.

Usiache kuja kwenye huu, uzi hata kutupa moyo. Sisi ambao bado.
Nasi siku yetu inakuja.
Ahsante sana mkuu, mimi nipo hapa ni nyumbani siwezi kupakimbia
 
Yaan kaka nimefarijika as if nakufaham kwa sura mzee baba[emoji3][emoji3], karibu sana kwenye Grid ya taifa ya asali . Hongera sana bro
Ahsante sana mkuu kwa kunikaribisha. Mimi ndio huyo kwenye Avatar jaribu kuzoom unaweza kunifahamu sura ya form one hiyo[emoji3][emoji3]
 
Back
Top Bottom