Nadhani la kuweka matokeo ya Oral kwa namba Ile Ile mtu aliyofanyia Written interview baada usaili wa mahojiano kuisha ingependeza, mtu unarudi nyumbani Huku unajua kama umefaulu au kutofaulu ungojee placement au lah yakupasa uendelee na safari za usaili Tena.
Kwani naona kinatokea kitu mtu umefanya oral lakini hujui kama utakuwepo ndani ya placement au haumo, katikati Tena unaitwa usaili a unaenda Huku hujui hatma yako ya mwanzo ikoje...
Wangetoa matokea ya Oral kwa namba hata kama watachelewesha placement ambayo itakuwa na Majina ya wahusika Haina tatizo naona,kwani mtu unakuwa unajua nafasi tayari ushapata utulie tu kusubiri PDF la placement....
Sekretarieti ya Ajira