Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Jidanganye tu, kuna usahili wa heslb, kuna jamaa alikua na bachelor ya public administration sijui ilikuaje akafanikiwa ku-apply na kuwa short listed. Tangazo lilitaka watu wa education na accounting, jamaa wakimzingua sana, na wakampa tangazo asome kama kozi yake ipo pale.
Kusema wanaangalia tu majina ni uongo.
Kozi inaweza isiwepo but kukawa na relevant qualifications au pia wanazinguaga kuhusu ilo kama kozi inakuwa haipo kwenye advert.

But nasikia pia unaweza kufanya usaili ukapita but usipewe kazi kutokana na sintofahamu ya cheti chako.
 
Mwanangu anadai yake ime change kuwa "Selected" kavu
Mkuu, Mimi saili yangu nilofanya November imebadilika huko kwenye APP Sasa imeandika "SELECTED FOR practical interview Hali ya kuwa Wala sikufanya hyo Practical interview 😂😂
 
Naimani watakuwa wamesikia kilio Cha Vijana wengi,maana unaenda kufanya Saili nyingi bila kujua Placement kama utakuwepo au hautakawepo.Mwisho wa siku unajikuta upo eneo la Usaili unasuburi Usaili unachungulia web unakuta Upo kwenye Placement,ni furaha unapata japo unakuwa umechoma nauli.....

Kama itakuonyesha selected for placement Huku hujui lini PDF itatoka lakini uhakika unakuwa nao,itakufanya usiombe Tena kazi na kuachia wengine waombaji waombe,na kama pia ulikuwa na usaili utaacha wengine waende wewe utatulia.Lakini pia kama baada ya Usaili utaona matarajio ya kuwemo kwenye Placement haumo itakufanya pia upambane kwa saili zijazo.Kama ambavyo huwa wanasisitiza yakuwa Kwa waombaji ambao hawakuona Majina Yao wasisite kuomba Tena...


Sasa Ili kuepusha watu kuomba omba kazi na kuwa na double placements au kukimbia taasisi....
Hili linawezekana kabisa kama itakuwa hivi baada ya muda Fulani vikao vya kuchuja Majina ya waliopangiwa vituo vya kazi kwenye Taasisi Mbalimbali...
Status zinaweza kuwa hivi....

-'SHORTLISTED'
-SELECTED for Practical Interview..Kwa wale wenye saili zenye Practical pia...
-SELECTED for Oral Interview..
-SELECTED for PLACEMENT.
-SELECTED for NULL....hapa mtu imuonyeshe asuburi kwa mwaka labda yupo kwenye Database kama nafasi ikitokea anaweza kupata....
-NOT SELECTED FOR NULL....Hii status ionyeshe ya kuwa mtu hajabahatika kuwepo upande wowote either Placement or Database kwa maana Ajaribu Wakati mwingine....
Mtazamo wangu tu uko hivyo nikiwa kama mwombaji wa Ajira kupitia PSRS..

Sekretarieti ya Ajira
Naunga mkono hoja
 
Back
Top Bottom