Hapa ndy nakosaga Nguvu watu tunasubiria matokeo nyie mna taarifa za watu kuitwa kazini
Ngoja nikushirikishe machache tu ambayo yanaendelea huku maofisini ujue jinsi Dunia ilivyokuwa haina USAWA....
Mimi binafsi ni mwaka wa 3 huu natafuta uhamisho (nishafanya Kazi miaka 10, kwahiyo Nina sifa zotee za kupata uhamisho) ila sasa...
Nikiwa na hustle na kutafuta uhamisho
1. Kuna watu wanapata Kazi (ajira mpya) wanakuja kureport, anarudi home kusubiri cheki namba.
Ile anaipata, hata hajaanza Kazi, anakuja na barua ya uhamisho kahamishiwa Taasisi fulani. Kwa halmashauri anatemana nayo kihivyo
UNADHANI HUYU HATA AJIRA ALIIPA NJIA KAMA YAKO?
2. Mmepata ajira mpya, wewe unawaza umfundishe Kazi ili umuachie ofisi uhame.
Na uhamisho hutoka baada ya mwaka wa ajira (ukishathibitishwa).
Ndani chini ya mwaka mtu anakuja na barua ya uhamisho na anasepa anakuacha wewe wa miaka hapohapo.
3. Siku umekaa unahili wala lile, unashangaa DED kamind. Kisa kapokea simu kutoka juuu huko "mtumishi fulani anatakiwa ahame haraka"
Braza hii Dunia japo Kuna Mungu, ila Kuna watu Wana WATU, sio watu ni WATU.
Mungu akujalie upate ajira, ipo siku UTANIELEWA.
Karibu kwenye Utumishi wa Umma.
#YNWA