Subira ni rahisi kuisema ila kuitekeleza ni ngumu, lakini ni muhimu sana kuwa na subira.
Nakumbuka tuliitwa interview written kwenye taasisi moja pale udom (CIVE) tarehe 06/09/2022 nikapita, tukaitwa oral 08/09/2022 tukafanya lakini watu wakaitwa kazini mwezi wa 12/2022 jina langu halikuwepo. Nikapotezea nikawa nafanya mambo yangu mengine ya papatu papatu ili nipate kulipa kodi ya chumba nilichopanga mjini dsm. Mnamo tarehe 29/03/2023 utumishi wakatoa mkeka na mimi nimo tena taasisi taasisi moja kubwa ya serikali iliyoshika namba 2 kama mwajiri bora tanzania.
Sikuwa najua, siku sina hili wa lile jamaa tuliyekutana dodoma yeye ni mkazi wa mbeya ananipigia simu nikiwa kimara mwisho nataka nipande daraja niende ghetto ananipigia simu ananipa hii taarifa na kulalamika kuwa amenitafuta tokea asubuhi sipatikani, ni kweli nikiwa na heka heka simu huwa naweka kindege, lakini jioni huwa natoa nikiwa narudi nyumbani nikaftur kwangu.
Akaniambia oya jumatatu twende dodoma tukachukue barua tumeitwa kazini, sikuamini nikajua mzaha, akasema nakutumia pdf ingia Whatsapp, kweli naona jina langu na lake limo, siwafichi almanusura nigongwe ma gari maana nilikuwa natizama pdf karibu kabisa na lami sasa ile kupagawa nikajikuta naenda kwenywe lami kati kati ila msamalia alinivuta shati kwa nguvu kuikwepa bajaji.
Jumatatu tulienda mara moja na tukachukua barua zetu na j4 kuziwasilisha kwa mwajiri wetu. Ndipo tukaanza msoto mpya unaoitwa vetting mpaka tarehe 29/05/2023 tukapewa barua za kuripoti vituo vyetu vya kazi.
Jamani sekretarieti ya ajira ni mkombozi, sina babu, baba wala shangazi aliyeko huko na mimi ndio wa kwanza kupata kazi serikalini, kikubwa ukifika hatua ya oral basi ipo siku yako tu isiyo na jina jitahidi kutembelea psrs. Laiti kama tassisi zingekuwa zinaajiri zenyewe nakwambia kweli, ni wenye konekisheni tu ndio wangepata kazi ila hawa utumishi wanahakikisha keki hii ndogo tunaila wote hata wewe ambaye kwenu hakuna historia ya mtu hata mmoja aliyewahi kuketi meza kuu na wafalme. Asanteni sana