Acha tu mzungu anajua kucare hawana longo longo za kikuda wala majivuno kama ma Hr wakibongo.Mbongo akiona mtu anataabika ndio roho yake inafurahi.
Sijawahi kufanya interview hata moja ila hii ya bomba la mafuta la east africa ndio imekuwa ya kwanza aloo mzungu mzungu tu.
Tulikuwa wengi tulioitwa kwenye interview almost 300 ila hata kama uko kijiji gani utalipiwa nauli hadi ufike dar kwenda na kurudi usafiri wowote utakaopenda ila usipande ndege tu[emoji3][emoji3].Hii ni kwa both oral and written.
Ukilala hotelini hata kama ni guest ya 5000 ,watakulipa 70,000 per night. Hotel tuliokuwa tukifanyia interview sasa ni seacliff [emoji3][emoji3]. Pesa ya kula 30,000
Na hapo Hotelin unakuta wamekuandalia Chai nzito vitafunwa vya kila aina, maji, chocolate,pipi yaani watakulazimisha ule hata kama hutaki utakula tu.
Hoteli ile ni kubwa ila kuanzia getini utakaribishwa kama mfalme. Kuna wale ambao kwa namna moja ama nyingine walikuwa wanashindwa kufika kwenye interview yaani utapigiwa simu wanakuuliza kama utaweza wakupangie siku nyingine. Kuna jamaa alisema siwezi kuja sababu sijajiandaa wakawa wanambebeleza njoo hivyo hivyo ujaribu bahati yako.
Maswala sijui ya kubeba mavyeti hawataki ni wewe na I'd yako yoyote. Ukimaliza interview unaenda kwa cashier anakulipa pesa zako zote ndio unasepa.
Kwenye oral interview kila mtu alikuwa amepewa saa moja kwenye venue uliopangiwa mfano ukachelewa wanam interview mwenzako aliewahi halafu wew watakuinterview baadae sio kama wabongo eti ukichelewa hata kwa bahati mbaya ndio imekula kwako na mabango juu.
Wakati wa interview sasa nilikuwa najiuliza nitaongea kizungu gani mimi na wazungu kwenye lisaa lizima wakati kizungu chenyewe sijui aloo wale jamaa wanajua kucare [emoji3][emoji3][emoji3]interview zote zingekuwa hivyo daa wakiona kuna swali unatapa tapa kujibu wanapredict unachojaribu kujibu wanakuolezea mpaka mwenyewe unasema yes yes yes ndio hiyo.
Au wakiona umechoka kidogo wanakwambia pumzika dakika tano kunywa maji Kisha tuendelee. Ambao tumepita oral interview last month tumeambiwa tutafute best private hospital yoyote iliyo kwenye mkoa uliopo Kisha tuwatumie ndio tunasubiri majibu yao twende kwenye medicals.
Sent from my SM-A025U using
JamiiForums mobile app