Ni kweli unachosema ila ni maamuzi Tu mkuu na mindset yako, kwa sababu usipoamua kupotezea na kumove on itakupa tabu sana ata kwenye kufanya maamuzi mengine ya kutafuta Ridhki kwa kuhisi Asali itaingilia kati
Mimi baada ya kufanya oral mwezi wa Kwanza na majina yakaanza kutoka mwezi wa 3, hadi wa 6 majina yanatoka tu ila langu kushney, nikaamua kumove on na Mambo mengine maana muda hauniruhusu Mimi kuendelea kuwasubiri utumishi
Nikaacha kabisa kuingia Ajira portal website hadi App, nikasahau kabisa ata kama nilifanya interview, nikaanza kutafuta kazi serious private sector na ilipofika mwezi wa 7 nikawa nimepata kazi private
na bahati mbaya au nzuri kufika mwezi wa 11 nikapigiwa simu na washkaji kunipa hongera wengine ata waga hatuongei wakinipa habari za placement imenikuta sipo kinyonge
Sasa sio mara zote utapata kazi private na Gavoo tena ikakukumbuka kwahiyo ni kheri ukajiandaa kisaikolojia kwamba ikija au isije fresh Tu ila angalau una shughuri halali inayosaidia mkono kwenda kinywani na kutatua shida zingine za kibinadamu