Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Haaah usijali majina yetu yako kwa Katibu siku ps akimpa asaini file mapema uko Miguelmungu atubariki na sisi aisee tusije tukabaki walinzi wa uzi
Usikate tamaa siku yako iko na inakuja si muda.Yani Kuna muda Hadi nawaza kwanini nilisomea mambo ya Ardhi. Kada tu kuiona kwenye Pdf ni kazi kweli kweli.
Wewe je??Wala usione tabu kabisa, zamu yako ikifika nitakupa hongera kama wengine ninavyowapa.
Mzee huyo broo wetu nadhani anamaliza mwaka kazini hawa ndo waliuchanganya Uzi na wakapata kazi woteWewe je??
Mkuu hata kama hujapata kwa wakat huu, usiache kuwapongeza waliopata...hii ni kama ridhiki, kila mtu na yakeWewe je??
Wewe je??
Finally I made it!
Kutana na Mwifwa- From three times defeat to Champion
Hii ndio ilikuwa safari yangu ya kusaka mrija wa Asali.
Mwaka 2021, safari hii ilishika kasi kwa kuapply mara 8( Sekta binafsi, Wizarani na Tamisemi). Kote niliangukia pua, Sekta binafsi sikubahatika hata kuitwa kwa usahili.
Mwaka 2022, kasi ikaendelea kushika kasi nilipoapply Wizarani na Tamisemi kabla ya kutimkia PSRS, mara hii niliangukia pua pia Wizarani na Tamisemi.
PSRS nilifanya application 5, 4 nikawa shortlisted, moja sikuwa shortlist kwa sababu isiyokuwa ya msingi maana hiyo sababu wangeizingatia nisingekuwa shortlist zile zingine 4.
Kwenye shortlist 4, tatu nikakandwa mfululizo hadi nikakata tamaa, ila wadau wa humu wakanipa moyo na nikapata nguvu ya kwenda kupambana.
Baada ya kwenda kwenye battle nikaingia oral kimasihara. The rest is history, what a joyful in my life history, my eyes are filled with joyful tears.
Join me in celebrating this remarkable history!!
Vuta subira kuwa na Imani mambo yatajiseti. Wapo wengi ambao walikuwa wanasema kama wewe ila baadae nafasi zikatolewa na wakazipambaniaYani Kuna muda Hadi nawaza kwanini nilisomea mambo ya Ardhi. Kada tu kuiona kwenye Pdf ni kazi kweli kweli.
Kweli kabisa Mkuu, seketarieti analaumiwa bure, watu hawajui budget zinavyosumbua…kuna jamaa angu jina lilitoka march 2022 akaanza kazi august yakeSuala la Placements lipo mikononi mwa Mwajiri.
Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa walifanya Oral June 3, 2024. July 15, 2024 placements zikatoka. Hapo mwajiri ana uhitaji na watu wake akaamua apelekewe mapema.
Hongereni wote mlioingia kundini, mkawe watumishi wema
Yani Kuna muda Hadi nawaza kwanini nilisomea mambo ya Ardhi. Kada tu kuiona kwenye Pdf ni kazi kweli
Kada nzuri sana izo mkuu, wakati wa Mungu ni wakati sahihi utatusua tuYani Kuna muda Hadi nawaza kwanini nilisomea mambo ya Ardhi. Kada tu kuiona kwenye Pdf ni kazi kweli kweli.
Hongera Sana mkuu, kuna Raha Fulani Ivi haieleziki hongera Sana Kwa kutimiza ndoto, ukawe mtumishi mwema na mwadilifu kila la kheri katika majukumu yako mapya ukachape kazi mkuuNasoma uzi nikiwa safarini hivi sasa kuelekea Asha Rose Migiro... Naona kama naota hivi kumbe kweli, wakuu tuendelee kupambana tusikate tamaa. Wakati wa Mungu ndio wakati sahihi
Kila la kheri mkuuNasoma uzi nikiwa safarini hivi sasa kuelekea Asha Rose Migiro... Naona kama naota hivi kumbe kweli, wakuu tuendelee kupambana tusikate tamaa. Wakati wa Mungu ndio wakati sahihi
Ni kweli mkuu ngoja tupambane kwenye interview mkuuMkuu hata kama hujapata kwa wakat huu, usiache kuwapongeza waliopata...hii ni kama ridhiki, kila mtu na yake
kaka tupeane asali mbona kama you have authority katika utumishi.Habarini Ndugu zangu wapambanaji.
Naomba kwa yeyote aliepata kazi au alieshikwa mkono akalamba asali, Sifa na Utukufu ampe Bwana, maana hata kama umeshikwa mkono ni Bwana katengeneza njia kwa huyo mtu alifanikishe.
pia tafadhalini msinitumie msg Pm, sijahusika kwenye Asali ya Pinaco, ila tu niliguswa sana na namna alivyokua aki appear humu kila siku na karibia kila page lazima awepo, mkumbuke humu ndani kuna watu mbali mbali wanapitia, wapo wanaochangia moja kwa moja, na wapo wasiochangia ila wanazipitia conversations zenu kwa uzuri.
Ni sawa na ule uzi wa bwana mdogo Rick Boy kuna siku nilistaajabu kusikia mtu akiuzungumzia nikiwa sehemu ambayo si rahisi kuamini kama yipo mtu wa jamii Forum.
I am just a normal guy, ilaa... kuna uwezekano kulingana na watu wa hapa na pale naowajua naweza washirikisha sikitiko la mtu flani sio mfano mtu mmoja au wawili na kama Mungu akijaalia mambo yanatiki.
Hivyo kwasasa nisitumiwe msg imetokea bahati tu kwamba nilimtaja Peanacco na kumbe Mungu alikua amekwisha achilia Baraka juu yake.
Nitoe wito kwa watu wenye nafasi na network wanaopitia uzi huu najaua wapo wengi na huwa hawasemi neno, basi ukiona kuna kijana umevutiwa au kuguswa na masikitiko yake emu mtext umsaidie, ANGALIZO, MSAIDIAJI AU MSAIDIWA USIOMBWE PESA AU KUTUMA PESA ILI USHIKWE MKONO HASA KWA MTU USIEMFAHAMU, NA KAMA ITAKUJA SWALA LA SODA UWE UMEJIHAKIKISHIA KWA UKARIBU NA UHALISIA WA ASILIMIA 70-80% KWAMBA KUNA HARUFU YA ASALI YA KWELI.
Nitoe hongera kwa wote wanaotoa shuhuda za kula asali, pia wazid kuelezea hatua za kupigiwa simu ilikuaje..kufata barua ilikuaje na kureport ilikuaje, ili kuwapa moyo na kuwaburudisha walio katika lindi la kucboka.
Sifa na Utukufu kwa Bwana Yesu atupae kufikia malengo yetu na kufungua njia zetu.