Marcellojr
JF-Expert Member
- Jun 29, 2021
- 298
- 773
Ujumbe na ushuhuda nzuri sana kaka,hongera pia sana ndugu....umeongea points muhimu kakaMwaka jana mwezi wa sita ilikuwa interview yangu ya kwanza kufanya nilimaliza chuo 2022.Kwa bahati nzuri Mungu akanisaidia nikaingia oral kwa mara ya kwanza.
Kimbembe ikawa ni kusubiria placement ...kwa kweli nilikuwa na kiherehere sana😅😅 ikawa kila siku nikulalamikia placement kwa nini hawatoi majina,nikaanza ku imagine siku nikiwa kwenye gari naenda kuchukua barua(ikumbukwe ni interview ya kwanza😂😂) basi nikawa moto na kila mtu home akawa ananipa matumaini ananiaminisha kwamba lazima utapata hii nafasi usihofu😅 nami nikaanza kujipanga kuanza kazi kama vile baba yangu ndiye anaeajiri watu kwamba mimi kupata ni uhakika...
Basi Mungu alivyo mwema mwezi wa 8 placement zikatoka kuangalia!!!.... too bad!!! sikuwemo nikahisi moyo kuvunjika sana maana expectation niliyokuwa nayo ilikuwa kubwa mno nikajipa moyo labda huenda ntapata kupitia database...baadae majina ya database yakawa yanatoka kila jina simo nikaanza kujikatia tamaa🤦🤦...baada ya Muda wakaacha kutoa majina kwenye database ya kada yetu kwa muda mrefu hapo ndo nikajua kabisa kuwa nilishakosa.
Basi nikawa nimekata tamaa na interview (japo nimefanya moja nilikata tamaa kulingana na maisha na gharama za kufanya interview dodoma) nikawa nimeridhia rasimi maisha ya kuwa mwanakijiji😅nikapoteza matumaini ikafika hatua mpaka nikaamua ku logout humu jf ili nisipost wala kucomment chochote.
Lakini Mungu alivyo wa ajabu jana pdf ya tarehe 20 nimeliona jina langu kwenye pdf kama utani tu yani😅😅😅(nina furaha kubwa sana na namshukuru Mungu)
Nilichojifunza ni kwamba kinachofanya maumivu ya kukosa jina lako kuwa makubwa ni kuwa na EXPECTATION KUBWA za kuamini kwamba utapata basi ukikosa unajikuta unaumia sana na kujiuliza maswali mengi.
...Niendelee kuwatia moyo ambao bado hamjafikiwa SIKU YENU ITAFIKA TUWEKE MATUMAINI KWA MUNGU NA KUPUNGUZA EXPECTATIONS TUTAFIKIWA TU🙏🙏