Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Nimekuja tenaaa...
Nyie mnajifanya hamtaki mambo ya pdf wakt likitoka wakwanza kuchek😀 ...tumepiga paper lazima tuulizie placement...
Psrs wametunawisha, watupe msos😀
 
Kwanza kabisa swali la kwanza Tell us about your education background
2. Swali la pili duties zako zile lakini hawakuulizi direct huwa wanaanza tofauti kidogo unaweza usielewe kama wanataka duties zile Kwahiyo kuwa makini usipaniki
3.Swali la tatu ujuwe challenge za kazi yako na hapa wewe ndo inabidi uoneshe unajua sasa na jinsi yakuzisolve hizo challenge
4.kuanzia la nne sasa hayo ni technical questions zinabase kwenye zile duties Kwahiyo isome kila duties uelewe inavyofanyika na kingine soma notes za course yako
Nadhani mpaka hapa mzee ukipita humu basi jiandae tu kwenda kuchukua barua
Hebu jaribu kuyafata haya yanaweza kukusaidia
Jamani wale wa Oral...piteni humu
 
Hahahaaa, nilikaribishwa kwa mkando heavy sana pale CIVE, kabla sijakaa vizuri nikatandikwa ndoige pale DUCE[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3], nikawa najisemea kumbe mambo ndio yako hivi. Nikirudi kijiweni nikiwa mnyonge, nilipoulizwa mambo yalivyoenda nikawaambia "nimekimbia" kwani mambo sio kitoto.

Muda huo mwenzangu ambaye niliambatana naye, alifika oral zote na nikamuacha akiwa anapambana na oral, mimi nikarudisha mpira kwa kipa(kijiweni), aliporudi sikuwa na mood ya kumuuliza nini kilichoendelea kule. Nilibaki kuwa mnyonge huku nikifikiria jinsi nafasi inavyotokaga kwa mbinde.

Nilipumzika wiki 1 nikaanza maandalizi ya kurudi UDOM, mara hii ilikuwa CBSL, huku tena nilichezea "Mandonga mtu kazi"[emoji3][emoji3][emoji3] huku mwenzangu akiendelea kupeta.

Kwenye Profile ikawa imebaki received ya NAOT huku nikiikatia tamaa kuanzia hatua ya kuitwa kwa mkando wa written. Nilirudi kuja kueleza hapa ila nasaha kutoka kwa majobless wa humu ikawa chorus ninayoimbiwa[emoji3][emoji3] hadi vina vikaniingia kwenye Oblongata na hatimaye shortlist ya NAOT ikatoka na nikawemo. Si nikaenda kujilipua kimasikhara[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3], cheche zikatua kwa wakandaji wa ana kwa ana ofisini kwao nikawa miongoni mwa wasubiri placement.

Sasa target yangu ni angalau niingie database, siku nikiona jina kwenye placement tutashereheka wote ushindi humu.

Kama tulianza wote kusubiri shortlists, tukakandwa, tukaimprove na kufika oral tukiwa tunashare feelings kwa pamoja, haitashindikana kusherehekea ushindi kwa pamoja.

#MkonoKwaMkonoHadiKwenyeMrijaWaAsali
Mwifwa wewe ni legend kabisa. Endelea kutujaza imani kaka. Watu tusikate tamaa, ona huku ulipotoka.
 
Mwenyewe nilikuwa sina habari kabisa siku hiyo na sikuingia humu kwa muda kama masaa kadhaa nyuma.

Nilipokuja kuwasha data nikaingia WhatsApp nikakuta jamaa kanitumia pdf na kunipongeza. Aisee Moyo ulilipuka sana nikiwa siamini kama, nikaidownload fast na kuifungua nihakikishe, nilipoona jina nilianza kutokwa machozi kabisa[emoji3][emoji3]
Hata mimi, sikuwa nimeingia mtandaoni muda kweli. Nakuja kushika simu napigiwa na watu kunipongeza. Ikifika siku unatafutwa wewe kupongezwa. El marabiosh na Utawala2025 msivunjike mioyo. Mtapigiwa simu na watu kuwapongeza. Nina uhakika na hili.
 
Nimegundua kitu kuhusu hizi placements.

Yaani zinapitia hatua ndefu hadi zije zitoke ndio maana tunaona zinachelewa sana.

Barua zetu zimeandikwa tarehe 8/12/2022(mwezi mmoja baada ya Oral) halafu placement imetoka tarehe 9/1/2023(mwezi mmoja baada ya barua kauandaliwa).

Je hiyo interval ya mwezi mmoja mmoja, nini huwa kinafanyika?

Turejee kanuni zao.

Baada ya Oral matokeo hukusanywa/alama zinakusanywa zinakuwa compile sehemu moja kama oral ilifanyika sehemu tofauti tofauti(yaani PSRS na Zenji). Then Mwenyekiti wa jopo la Panelist atakabidhiwa hayo matokeo na yeye atayawasilisha kwenye Board ili placement zikapangwe kulingana na ufaulu wa oral.(hapo mwezi ushakatika).

Mwezi mwingine inakuja suala la kusainiwa, Hapa mzee Kitenge atatenga muda wa kuzisaini barua zote zilizoandaliwa, hadi kumaliza mwezi ushakatika.

Baada ya hapo ndio zamu ya placements inafika, ikitoka tu barua ziko tayari ndio maana kuchukua barua haichukui muda ni dk chache tu.

Kwa hiyo mnaosubiri placement inabidi mtambue hilo na subira ndio silaha ya kuishi nayo katika hicho chote
Mi mjumbe tu wakuu. Hili nalo neno
 
Finally I made it!

Kutana na Mwifwa- From three times defeat to Champion

Hii ndio ilikuwa safari yangu ya kusaka mrija wa Asali.

Mwaka 2021, safari hii ilishika kasi kwa kuapply mara 8( Sekta binafsi, Wizarani na Tamisemi). Kote niliangukia pua, Sekta binafsi sikubahatika hata kuitwa kwa usahili.

Mwaka 2022, kasi ikaendelea kushika kasi nilipoapply Wizarani na Tamisemi kabla ya kutimkia PSRS, mara hii niliangukia pua pia Wizarani na Tamisemi.

PSRS nilifanya application 5, 4 nikawa shortlisted, moja sikuwa shortlist kwa sababu isiyokuwa ya msingi maana hiyo sababu wangeizingatia nisingekuwa shortlist zile zingine 4.

Kwenye shortlist 4, tatu nikakandwa mfululizo hadi nikakata tamaa, ila wadau wa humu wakanipa moyo na nikapata nguvu ya kwenda kupambana.

Baada ya kwenda kwenye battle nikaingia oral kimasihara. The rest is history, what a joyful in my life history, my eyes are filled with joyful tears.

Join me in celebrating this remarkable history!!
Haya jamani....mi mjumbe tu. Tuishi humu
 
Hata mimi, sikuwa nimeingia mtandaoni muda kweli. Nakuja kushika simu napigiwa na watu kunipongeza. Ikifika siku unatafutwa wewe kupongezwa. El marabiosh na Utawala2025 msivunjike mioyo. Mtapigiwa simu na watu kuwapongeza. Nina uhakika na hili.
hivi nyie mlipatajepataje mbona mbinde hivi jamani au mlioga dawa khaa 🤣 🤣
 
Back
Top Bottom