Kwa mujibu wa maelezo, inaonekana kuwa wizara ya afya baada ya kuwa imepewa kibali cha kuajiri ikaona hakuna haja ya kutangaza ajira wakati kuna watu kibao kwenye database ya PSRS. Kwa hiyo ikaomba ipewe watu kutoka database. Kwa maana hiyo hao walioitwa ni kutoka database hadi waliowekwa database baada ya usaili wa kada ya afya hivi karibuni. Ina maana waliopangiwa post baada ya usahili wa afya bado hayajatangazwa!! Unaona mambo ya Mungu hayo!! Aliyeko database anamtangulia aliyepata placement, tena anapelekwa hospitali za rufaa, mikoa na taasisi!! Aliyepata placement ni wa halmashauri!