Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Kwahio walio omba kazi hivi karibuni waji andae tu na wao kuitwa kwenye usahili mwezi wa saba maana kazi ipo inavyo onekana kule..😄
Wanaweza kuitwa ata baada ya mwezi mmoja mbona kuna kazi zimetangazwa mwez wa kumi na washafanya tayar
 
Endeleeni kusoma mjiandae vyema hakuna kitu kinauma kama kukamdwa imagine umesubili muda wote huu. Interview unaitwa unaishia written mazee

Unaona unachelewa kuitwa ila ukiitwa zibakia siku mbili kabla ya mkando unajiona namna gani haujajiandaa vizuri..
 
Napita hapa kutoa shukrani kwa wote wanaoendelea na waliochochea kutupa watu moyo tuendelee kuongeza received humu. Nami Mwenyezi Mungu ameamua wakati wangu umefika. Nashukuru Mungu nimeitwa Dodoma kuchukua barua. Nilianza mchakato wa kupambania ajira tangu mwaka 2021, bahati mbaya sikuwa na uwezo wa kuhudhuria zote nlizoomba. Kuna kipindi nilikata tamaa maana mikando ilikuwa ya kutosha na ndio nikajiunga jf kuangalia wadau wanasemaje kuhusu swala la ajira. Hatimae nikakutana na huu uzi na comment za wadau kuhusu kuendelea kupambana.
Mwaka jana nimefanya interview moja nikafika nayo oral na japokuwa nilikosa post niliyoomba jana mkeka umetoka nikiwa nimepangiwa ofisi nyingine.
Nashukuru sana Mungu na watu wote ambao japo wamepata kazi bado wanarudi humu kuwapa wapambanaji wengine moyo.
ahsanteni
Tukizimiss sana shuhuda za hivi.

Umetufungulia mwaka kwa shuhuda nzuri sana.

Hongera sana kwa kupambana, pia hongera sana kwa kuingia kundini.

Kila la kheri ukawe mtumishi mwema.

Kwa ambao bado mpo kwenye foleni, slogan ni ile ile, hakikisha unaongeza received kama una sifa, hakikisha unahudhuria mkando bila kukosa, hakikisha unapambana hadi Oral then muachie mgawa riziki afanye yake.
 
Back
Top Bottom