Napita hapa kutoa shukrani kwa wote wanaoendelea na waliochochea kutupa watu moyo tuendelee kuongeza received humu. Nami Mwenyezi Mungu ameamua wakati wangu umefika. Nashukuru Mungu nimeitwa Dodoma kuchukua barua. Nilianza mchakato wa kupambania ajira tangu mwaka 2021, bahati mbaya sikuwa na uwezo wa kuhudhuria zote nlizoomba. Kuna kipindi nilikata tamaa maana mikando ilikuwa ya kutosha na ndio nikajiunga jf kuangalia wadau wanasemaje kuhusu swala la ajira. Hatimae nikakutana na huu uzi na comment za wadau kuhusu kuendelea kupambana.
Mwaka jana nimefanya interview moja nikafika nayo oral na japokuwa nilikosa post niliyoomba jana mkeka umetoka nikiwa nimepangiwa ofisi nyingine.
Nashukuru sana Mungu na watu wote ambao japo wamepata kazi bado wanarudi humu kuwapa wapambanaji wengine moyo.
ahsanteni