Kila mwenye sifa aliyewahi kufanya usahili na akafaulu ana haki ya kupangiwa kituo cha kazi nafasi zikipatikana.
Hivyo basi hao waliowahi kufanya ndio wanabahatika kupangiwa kazi kwa sasa.
Pia, hawa walimu wanaoendelea kufanya sahili, wale wote watakaofika oral na kufaulu, kuna wapo watabaki database na watapangiwa nafasi baadae zilipatikana.
Mfano: Hawa wanaotolewa database huenda kunawapo walifanya sahili za nafasi ya kazi NECTA kama Examination Officer, Quality Control Officer, Quality Assurance Officer ila wakapangwa kufundisha.
Halafu hawa watakobaki database wanaweza kuja kupata nafasi baadae sehemu zingine palipo pazuri zaidi mfano huko NECTA na kwenye Vyuo vya kati.
Hivyo hapa ni ishu ya kucheza na bahati unaweza kuangukia popote.