Sole Proprietor
JF-Expert Member
- May 25, 2018
- 223
- 254
Na Arusha kuna Idd Mkuluu na Rama Mkuluu mmoja wao ameshatangulia kwa changamoto za kupumua pamoja na kampani yao. Wametumiwa sana na Gambo na CCM kuumiza watu. Kuchoma watu visu lilikuwa jambo rahisi kwao kuliko hata kumenya chungwa.Vijana wengi hasa wasio na ajira waliingia CCM sio kwa kukipenda chama bali kutafuta ridhiki na ajira za upendeleo ndani ya chama na serikali, huku role models wao wakubwa wakiwa akina Makonda, Polepole, Hapi, Mwigulu, Gambo, Sabaya, Murro, Shaka, Musiba, Habibu na wengine wengi.
Mienendo na tabia ya uongozi wa vijana niliowataja ilijulikana wazi ambayo ilikuwa ubabe, jeuri, fitina, dhulma, utekaji, mauaji nk, walitumia mbinu hizi hasa kuwadhalilisha wapinzani, wakosoaji na wafanyabiashara, wakajiona wao ndio Tanzania na Tanzania ni wao, wakasahau kuwa aliyewapa madaraka na jeuri hizo hana garantii na Mungu.
Kipindi cha utawala wa Mwendazake ili uteuliwe sifa kuu mojawapo ilikuwa ubabe, roho mbaya, matusi, jeuri, ilifikia wakati mwana CCM au polisi akimvunja mguu mpinzani anapongezwa pengine kupandishwa cheo.
Vijana wengi wa CCM wakaanza kuiga matendo na vituko vya akina Sabaya & Co, siasa chafu ambazo uchafu wake hata waonyeshwe kwenye video wanajifanya hawauoni, wakaiga vituko hivi ili waonekane wawafurahishe wakubwa zao wateuliwe, leo wameanza kukata tamaa baada ya kuona Mama hana siasa hizo chafu.
Baada ya kugundua hilo wanachofanya sasa ni kuwatetea role models wao wanaotenguliwa ambao walikuwa wateule wa mwendazake (Bashiru, Polepole, Biswalo, Sabaya), wameanza kumlaumu Mama wakitumia ilani ya chama kama ngao yao kuwa mama anaonyesha kushindwa kuitekeleza, huku lengo kuu ni kutaka kumshinikiza mama aendeleze ubabe wa mtangulizi wake siasa ambazo walitegemea kuja kunufaika nazo.
CCM Mwacheni Mama afanye kazi msimshinikize zamu ya Mwendazake imekwisha. Kazi iendelee.
CCM ilitengeneza laana ambayo tulikuwa tunakaribia kuishindwa kabisa kama Mungu asingeingilia kati.
Huyo sabaya akiwa uvccm Arusha alikuwa na kitanmbulisho feki cha usalama wa taifa. Badala ya kuadhibiwa kapandishwa cheo.
Makonda kampiga mzee Warioba badala ya kuadhibiwa kapandishwa cheo. Mnyeti hivyo hivyo.
Huyo sabaya anadaiwa madeni yakutumia vinywaji na kulala hotelini karibu kila hoteli Arusha na ukimdai anakutishia kukuumiza. Hatakiwi kuwa nje wala kuwa huru.