Kwanini vijana wengi wa CCM wanatetea siasa chafu za Sabaya?

Na Arusha kuna Idd Mkuluu na Rama Mkuluu mmoja wao ameshatangulia kwa changamoto za kupumua pamoja na kampani yao. Wametumiwa sana na Gambo na CCM kuumiza watu. Kuchoma watu visu lilikuwa jambo rahisi kwao kuliko hata kumenya chungwa.

CCM ilitengeneza laana ambayo tulikuwa tunakaribia kuishindwa kabisa kama Mungu asingeingilia kati.

Huyo sabaya akiwa uvccm Arusha alikuwa na kitanmbulisho feki cha usalama wa taifa. Badala ya kuadhibiwa kapandishwa cheo.

Makonda kampiga mzee Warioba badala ya kuadhibiwa kapandishwa cheo. Mnyeti hivyo hivyo.

Huyo sabaya anadaiwa madeni yakutumia vinywaji na kulala hotelini karibu kila hoteli Arusha na ukimdai anakutishia kukuumiza. Hatakiwi kuwa nje wala kuwa huru.
 
Sabaya ni duplica ya mwendazake ingawa huyu dogo amepitiliza kidogo ili kujinufaisha ...Hai padogo sasa uwanja mpana kucheza hizo siasa chafu alikosa akawa anavuka mopaka kwa nguvu zote kisingizio uhujumu na connection Mbowe maana aliwekwa kazi moja kuhakikisha Mbowe hapumui kamwe
 
Hawa vijana walikuwa "kazini" jiulize, Mojaa anajulikana kabisa kuwa ni jambazi,ameshakuwa na kesi za mauaji pia,ni kiongozi wa uvccm,amejenga gorofa kwa kazi hiyo hiyo ya kukata watu mapanga na ujambazi,analipiwa ada ya mazoezi ya viungo pale Life gym uzunguni na ccm,wewe unataka kuniambia ungepewa wewe hiyo kazi ya 'usabaya' ungeikataa?
 
Dhuluma ya ccm na mwendazke kisa tu hawataki upinzani Tanzania kwa namna yoyote ile.
 
amina na Mungu asikilize mombi yetu
 
Njaa
 
 
Hao siyo vijana wa UVCCM bali ni vijana aliowanunua na anawalipa Sabaya mwenyewe kwa kupost.

UVCCM sasa hivi wanajipanga upya na CCM mpya, wanakwenda na upepo
 
Mkuu Bams ulipotea sana, tumemiss madini yako. Nimefarijika kusoma post yako leo
 
Ccm ilishakufa inabebwa kwa nguvu ya dola hawana ushawishi wa hoja zaidi ya kumwaga damu zetu
 
Hao ni wachumia tumbo wasio na maadili. hawana hata chembe ya adabu...walikuwa wanaona raha kuwadhalilisha wazee hadharani. Wakae kwa kutulia chama kinarudi katika misingi yake ya utu na kuheshimiana.
Hawa vijana walioaminiwa ndio wamekivuruga chama na nchi kwa ujumla.
 
Hatuko salama hata sasa kwani kuna uwezekano mkubwa wa kurudi kwenye utawala wa aina ya mwendazake.

Imagine tuna watu kama mwigulu,dkmpango,Majaliwa ambao wana nafasi ya kuweza kugombea kupitia chama chao kama mazingira yakiwaruhusu,bila katiba mpya we are still fucked.
 
Si Wote.....

Binafsi simuungi mkono....

Siasa za KIHASAMA kupitiliza ni UPUMBAVU NA USHAMBA....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…