Kwanini vijana wengi walioharibika waliolelewa na mzazi moja hutokea upande wa single mama?

Kwanini vijana wengi walioharibika waliolelewa na mzazi moja hutokea upande wa single mama?

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Kuna wanaokuwa vizuri lakini tuwaangalie wale walioharibika

Husika na kichwa cha habari,

Katika wale vijana kuanzia miaka 15 ambao kimaadili wameharibika, ni kwanini wengi wamelelewa na single mothers?
 
Sababu ni hizi

1) Kudekezwa sana

2) Mama kuwa Busy na kazi na kutomlea Mtoto vizuri.

3) Mtoto kuwa na Chuki na Baba, hali hii upelekea Mtoto kuathirika kisaikolojia na kuwa na vitabia vya hovyo.

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
Mmonyoko wa maadili una sababishwa na factors mbalimbali ingawa malezi ya upande mmoja yanachangia pia.

Tusiwaseme ma single mother vibaya wajamene hadi wajione hawana thamani.

Malezi ni ya kwetu sote, kuanzia jamii, familia, ukoo, majirani. Dunia imebadilika na utandawazi ndio balaa zaidi.
 
Mama ana huruma in NATURE, so hawezi ku-enforce discipline kwa Mtoto.

Japo wapo kina Mama wanavaa viatu kwelikweli, hawataki Ujinga. Ila ni wachache.

MWISHO, Jamii imeharibika so mtoto analelewa vizuri ila anakuja kuharibika ukubwani.

Hii CHINI ni mfano wa kideo ya Binti aliyelelewa vizuri ila JAMII inaonekana inaenda kumharibu siku za usoni.

 
Mi nina chalii wa miaka miwili.. huwezi amini mama yake licha ya kuongea kwa ukali dogo huwa anakama kumzoea ila kuna muda nasema tu fanya hivi dogo anafanya chapu kitu ambacho kaambiwa dakika 3 zilizopita hakufanya.. bila sauti ya kiume aisee sipati picha mtoto atakuwa vipi na hasa wa kiume.
 
Mi nina chalii wa miaka miwili.. huwezi amini mama yake licha ya kuongea kwa ukali dogo huwa anakama kumzoea ila kuna muda nasema tu fanya hivi dogo anafanya chapu kitu ambacho kaambiwa dakika 3 zilizopita hakufanya.. bila sauti ya kiume aisee sipati picha mtoto atakuwa vipi na hasa wa kiume.
Sauti ya baba ni sauti ya msingi sana, trust me!
 
Husika na kichwa cha habari,

Katika wale vijana kuanzia miaka 15 ambao kimaadili wameharibika, ni kwanini wengi wamelelewa na single mothers ?
Wakati mwingine mama anataka kuonekana ni mwema sana kwa mtoto ili baba aliyewacha aonekane hovyo zaidi.So mtoto anakuwa kama yai flan hiv kwa mama.baadaye mtoto anaanza kuwa na sauti kwa mama.
 
Husika na kichwa cha habari,

Katika wale vijana kuanzia miaka 15 ambao kimaadili wameharibika, ni kwanini wengi wamelelewa na single mothers ?
Ungeandika single parents, ingependeza zaidi!! Tusiwe gender blind society!!
 
Husika na kichwa cha habari,

Katika wale vijana kuanzia miaka 15 ambao kimaadili wameharibika, ni kwanini wengi wamelelewa na single mothers ?

Kina Obama wamelelewa ni single mothers wakawa marais wa marekani.
 
The fact ni kwamba mwanamke mwenyewe inabid alelewe na aongozwe maisha yake yote, sasa huyu aje amlele mtoto peke ake lazima achemke tu.
 
Nionyeshe kijana yeyote aliyelelewa na baba yake pekee na amenyooka. Sijawahi ona.

Kuna mshikaji mmoja ni fundi malaya kama nini. Wiki jana alitoka na mtoto wake wa miaka miwili akaenda bar na uko akaenda lodge na malaya wakalala, mtoto akawasumbua asubuhi yake wakamleta kumlaza nyumbani kwa mlevi mwenzao (chumbani kwake) na wakamkabidhi mtoto kwa house girl. Siku ile pia yule jamaa akaenda kulala na malaya akaacha mtoto kwa house girl wa mtu baki.

Mama wa mtoto aliachana na mume, mama muda huo alikuwa hospitali anauguza mama yake hivyo mtoto akamuachia baba. Baba akakerwa na kubaki na mtoto akaendelea na ratiba zake bila bugdha.

Bora kumuacha mtoto mdogo kwa mama kuliko kwa baba.
 
Husika na kichwa cha habari,

Katika wale vijana kuanzia miaka 15 ambao kimaadili wameharibika, ni kwanini wengi wamelelewa na single mothers ?
Mtoa hoja sijajua lengo lako kuu hasa ni nini, lakini pasipo shaka umelenga kuwakejeli single mothers. Unachokikusudia na kutaka kuwaaminisha watu sio kitu kizuri na pia yapaswa ujirekebishe.

Mtoto anaweza kulelewa na wazazi wote wawili lakini bado wakaharibikiwa kwa maana ya kutokuwa na maadili mema yanayofaa katika jamiii na sio kwa huo mtazamo wako hasi juu ya single mothers.

Pia tambua kuwa kuna watoto ambao wanalelewa na single father na bado hawana maadili yanayofaa kwa jamii, na wapo wenye maadili, the same as to other children from single mothers.

Kuna factor nyingi zinazosababisha watoto kulelewa na single mothers alone, among them are the following:
  • Kuondokewa na baba ili hali mtoto au watoto bado wakiwa wadogo.
  • Kutalikiana (divorce) kati ya mume na mke. Mwanamke mwenye akili na upendo kwa watoto hawezi acha mtoto au watoto wake walelewe na baba yao kwa sababu lazima ataoa mwanamke mwingine and likely that woman may not care about other children kwa maana watoto atakao wakuta kwa mume, japo sio wanawake wote wana roho ngumu kwa watoto wa wanawake wenzao.
  • Kupata ujauzito pasipo kukusudia, na kuamua kuzaa mtoto pasipo kufanya ujinga wa ku-abort. Wanawake wengi wenye hofu ya Mungu hawapo tayari kutoa mimba (dhambi kwa Mungu) hivyo huamua kuvumilia mapito yote ya dunia for the sake ya kumlinda kiumbe aliyepewa na Mungu. Wanawake hawa wana maua yao peponi kwa sababu ndio ambao wengi hukejeliwa na kutukanwa na jamii inayowazunguka kisa tu eti wamezaa bila ndoa au kabla ya ndoa. Hawa wanawake hujifunga mkanda na kulea watoto wao pasipo kujali kejeli, dharau, manyanyaso n.k
  • Pia kuna wanaume kazi yao ni kutia tu mimba wanawake au watoto wa watu kisha kuwakimbia na kuwatelekeza. Hii pia ni sababu kubwa ya hawa dada zetu kuonewa na kuitwa majina ya ajabu lakini causative mkubwa ni mwanaume au wanaume kwa kushindwa kuzuia tamaa zao au kuwarbuni watoto wa watu kisha kuwatelekeza. Wanaume wengi wa hovyo wa aina hii wapo kila mkoa na kila kabila au jamii. Walaaniwe kwa huo uchafuzi wao.
  • Mwisho japo sio kwa umuhimu ni UBAKAJI KWA WANAWAKE. Wapo wanawake ambao hubakwa na wanaume na mwisho wa siku hushika mimba. Hili limewaumiza na linawaumiza wanawake wengi sana hasa teenagers (10 - 19-year-old girls). Linapotokea jambo kama hilo wazazi huamua tu kumsihii binti avumilie kisha azae. Katika hili wanafunzi wengi wa kike wamekatishwa masomo yao na kuishia kuwa single mothers.
NB: Tusiwanyanyapae single mothers. Tambua pia kuna single fathers.
  1. Wanaume tuache unyanyapaa kwa single mothers, badala yake tuwatie moyo kwa kusimama imara kulea watoto wao.
  2. Leo hii wapo wanawake wengi wanateseka kwa kutokuwa na watoto na umri umeshaenda na mayai yote yameisha au kupukutishwa na abortion nyingi walizokuwa wanafanya ila imebaki SIRI KUBWA ndani ya mioyo yao huku wakiugulia maumivu makali ya kutobarikiwa watoto.
TAFADHALI: NARUDIA TENA - NAOMBA TUWAPE MAUA YAO SINGLE MOTHERS WOTE HASA WANAPO UAGA MWAKA HUU 2023 NA KUUKARIBISHA MWAKA MPYA 2024 AMBAO TUNAOMBA KWA MUNGU BABA WA MBINGUNI UWE MWAKA WA HERI KWA SINGLE MOTHERS WOTE.
 
Mtoto anaweza kulelewa na wazazi wote wawili lakini bado wakaharibikiwa kwa maana ya kutokuwa na maadili mema yanayofaa katika jamiii na sio kwa huo mtazamo wako hasi juu ya single mothers.
Tatizo hujaelewa swali, wahusika ni wale watoto waliolelewa na mzazi moja na wakaja kuharibika
 
Kuna ex wangu mmoja wametengena na mume wake na ana mtoto wa kike.

Siku nmeenda toto muda wote linaweza tv tu,
Lina lialia eti ninunulie kifurushi cha kingamuzi na limekalili bei zote za vifurushi.

Yani akianza kufuatilia tamthilia utafikiri mtu mzima, lina wajua waigizaji wote wakati liko darasa la nne tu.

Nilipoona kelele za ninunulie kifurushi zinazidi nikaondoka zangu nikamwambia naenda kuweka hela kwenye simu nilipie.

Kama masaa 3 mamake anapiga simu eti vipi hicho kingamuzi.
.
Nikamchana, nikamwambia huyo mtoto unapaswa kumpeleka twishen siyo tv hapo unalea bomu.
 
Back
Top Bottom