Kwanini viongozi wa Iran wanauwawa na Israel

Comred Mbwana Allyamtu

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2016
Posts
362
Reaction score
909
KWANINI VIONGOZI WA IRAN WANAUWAWA NA ISRAEL.

Na. Comred Mbwana Allyamtu-CMCA
Monday -16/06/2025
Marangu Kilimanjaro Tanzania.

Pengine hili ndio swali la msingi la kujiuliza, toka mwaka 2023 Israel imefanikiwa kuwauwa viongozi wa juu kabisa wa Iran kwa kasi kubwa na kwa ufanisi mkubwa sana, kila pigo la Israel limekuwa on target kwa ufanisi, nini hasa sababu ya hili kufanikiwa?

Je ni kwamba Iran ni nyepesi kiasi hicho? Au viongozi wao awana ulinzi wa kutosha (VIP protection). Kama ndio inawezekanaje taifa kama Iran lenye uwezo mkubwa wa kutengeneza makombora ya masafa marefu ishindwe kilinda viongozi wake wa juu na muhimu?

Swali la pili inawezekanaje Israel kuingia Iran au sehemu yoyote inayo lindwa na ulinzi wa Iran ika ua viongozi wa juu wa Iran na kuondoka kirahisi? Na swali la tatu inakuwaje Israel kwenye mashambulizi yake inafanikiwa kuwauwa viongozi wa juu wa Iran? Tena on target?

Maswali kama haya najuwa watu wengi ujuuliza sana, sasa leo ntaeleza kwanini Israel inafanikiwa kwenye hili, wachambuzi wengi awaelezi hili, lakini ni muhimu sana kuelewa kwa namna ambayo Israel inafanikiwa kwenye hilo.

Kwanza zipo njia mbili ambazo Israel imefanikiwa sana kuwafikia viongozi wa juu wa Iran, njia hizo ni zifuatazo..

Moja ya njia hiyo ni Geospatial intelligence, yani ujasusi wa kutumia setilaiti ya kijasusi kupata taarifa au kuzituma taarifa, hii ntaileza kwa kina leo, lakini pia Israel hutumia njia nyingine itwayo "Dedicated Hacking system" hii ni njia ya Kudukua mifumo ya mawasiliano kimkakati. Zingatia hii ya pili ntaieleza pia na ndio njia ambayo imefanikiwa pakubwa kuwamaliza viongozi wengine wa Hizbullah na Hamas, twende pamoja sasa.

Geospatial intelligence...

Hii njia ya kijasusi ambayo utumia mfumo wa setilaiti kuchakata taarifa na kuzichora kijasusi yani "intelligence Maping" kwa ufanisi wa juu zaidi ya setilaiti, kisha taarifa nyeti ambayo imesha chakatwa utumwa kwenye eneo husika kwa matumizi ya kikachero.

Pia maafisa kipenyo huwa na passway maalumu ambayo wanaweza kuweka taarifa na kwenda moja kwa moja kwenye setilaiti kisha mifumo yenye ufundi uchakata taarifa na kuzichora na kuzituma eneo husika.

Sasa basi,

Maafisa kipenyo wanao tumia Mossad waliopo Iran ukusanya taarifa zote zenye uhakika za kuhujumu serikali kisha wanazituma kwenye setilaiti ya Marekani iitwayo (reconnaissance satellite) hizi setilaiti Marekani anazo takribani 16 ambazo utumia majina ya "KH" na setilaiti inayotumika kijasusi mashariki ya kati huitwa KH-4B hii ufanya kazi maalumu iitwayo "SIGINT" yani kupokea taarifa za intelijensia ya habari na mawasiliano ya kidigitali kisha kuzichakata na kuzigeuza kuwa alama za kijasusi (signals intelligence) na kutuma picha mkakati kwenye idara ya ujasusi Marekani iliyopo California kwenye kambi ya Vandenberg Air Force Base inayoitwa "Delta IV.

Taarifa hizo kisha utumwa kwa makachero wa Mossad, Mossad ndio utumia hizo taarifa kufanya mashambulizi on target, nini hufanyika sasa, Mossad wakisha pokea taarifa hizo ambazo huonesha maeneo yote ya kimkakati, wakati wanafanya mashambulizi utumia taarifa alama za ujasusi zinazo ongozwa na setilaiti ya Marekani HK-4B ambayo huonesha matukio yote yanayoendelea eneo husika wakati huo.

Kwaiyo Israel ulenga maeneo ya kimkakati ambayo viongozi wa juu wa Iran wanakuwa wapo, mfumo huu ni ngumu sana kuudhibiti kwasababu unaendeshwa na setilaiti, njia pekee ya kuudhibiti ni kuzuia ujasusi wa ndani ya Iran usiingiliwe na pandikizi kwasababu mfumo huu ili ufanye kazi kwa ufanisi unategemea taarifa za siri zilizo vujishwa.

Huu ndio mfumo ambao Israel inawauwa viongozi wa juu wa Iran kama kuku, ni kwasababu inapata taarifa zote nyeti za viongozi wa juu wa Iran wanavyo ishi, na kila kitu wanacho fanya.

Ndio maana Israel inathibutu kusema kuwa inaweza kumuuwa kiongozi mkuu wa Iran Ayatollah Khameneh kwasababu tu ina uhakika kuwa ina taarifa zake zote za kila kitu anachofanya na anapo ishi, kwaiyo ikitaka kummaliza ni ku-command setilaiti ianze kumfuatilia kisha kuweka target kumbola imfate alipo wakati huo.

Njia hii ndio ilitumika kuwauwa viongozi wa shambulizi la siku ya Ijumaa.

Mbinu hii Israel hutegemea Marekani karibu kila kitu na Marekani hufanya hivi kuzingatia mikataba ya kuilinda Israel kiintelijensia kwa mujibu wa mikataba ya "Mutual Defense Assistance Agreement wa mwaka 1952", na mwingine wa "General Security of Information Agreement wa mwaka 1982", na ule wa "Mutual Logistics Support Agreement wa mwaka 1991".

Mikataba hii yote inapigilia mikataba mama ya Marekani kuilinda Israel kuanzia ule wa Washington Accord na ule wa Sykes-Picok agreement.

Sasa basi...

Njia ya pili ambayo Israel uwapukutisha viongozi waandamizi wa Iran ni ile ya Udukuaji mifumo ya mawasiliano yani "Dedicated Hacking system".

Dedicated Hacking system....

Hapa pia Mossad udukua simu za mkononi pamoja na mawimbi ya Wi-Fi ya kompyuta za viongozi wa Iran, hapa makachero wa Mossad walio Iran ufanya kazi muhimu ya ku-activate mfumo wa Cybersecurity Performance Center (CPC) ambao utuma taarifa kwenda "Hacking Lab" iliyopo Mossad.

Mfumo huu una-activate vinasa sauti na camera na simu na kompyuta kisha Mossad unasa mawimbi ya Wi-Fi ya kompyuta au simu mahali ilipo, na kufahamu location husika kisha kutoa confirmation kwa marubani wa stealth fighter jet ya jeshi la Israel aina ya F-35 ambayo inakuwa angani pasipo kuonekana kwenye rada za Iran na kupiga bomu la PGM na kuua mlengwa wanaye muhitaji.

Kwaiyo wanapotaka kufanya shambulizi kwa njia hii ndege za kivita huwa stand by kusubiri confirmation ya mahali mawimbi yalipo.

Njia hii ilitumika kumuua Saleh Al-Arouri kiongozi namba mbili wa Hamas, mwanzilishi wa tawi la kijeshi la Hamas, Al-Qassam Brigade na Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Shura la Hamas.

Pia utaratibu huo wa Kudukua mifumo ya simu na vifaa vya kompyuta ulitumika pia kutamatisha Jenerali Qasem Soleimani, militaty strategist mahiri wa kusifika mashariki ya kati yote, wa nchi ya Iran ambaye aliuwawa pia na Israel mwaka 2020 nchini Iraq.

Kwaiyo makachero wa Mossad upokea taarifa nyeti kutoka CIA, mafunzo na mifumo utumia ya Marekani, ndio maana tunasema kuwa huwezi kutenganisha Israel na msaada wa Marekani kwenye ujasusi na kijeshi, haipo hivyo bahati mbaya, mkakati wa Geopolitical na Geostrategic Feed ulazimisha Israel kulindwa pale mashariki ya kati.

IRAN inaponzwa na idara yake ya ujasusi imeoza, Mossad imepandikiza makachero wengi wanao imaliza Iran, uozo wa idara yake ndio chanzo cha viongozi wake kuuwawa.

Inaendelea...

20250616_142733.jpg
 
FB_IMG_1750101749792.jpg
 
Back
Top Bottom