Kwanini Vodacom huwa wanaiba salio la mteja?

Kwanini Vodacom huwa wanaiba salio la mteja?

kagoshima

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2015
Posts
2,887
Reaction score
5,687
Wadau habari? ukweli ni kwamba, hawa vodacom, ukiingiza salio bila kujiunga na kifurushi basi hilo salio wanalipiga juu kwa juu.

Imenitokea mara nyingi. naweka salio ili niweze kutumia simu banking bila hata kutumia baada ya mda naona salio hamna. kwanini ninunue vocha kwenu halafu mniibie salio bila hata kutumia?
 
Huo ni wizi nenda kashtaki kituo cha polisi karibu yako
 
you might be true my friend!

Several time imenitokea, data ya bundle yangu imeisha, nanunua vocha nikiweka (NAZIMA DATA KABLA KUWEKA), nikitaka kuunga bundle naambiwa salio halitoshi! Mara nyingi sana imenitokea hii

Mfano jana tu!
bundle limeisha, nikazima data nikaweka vocha ya 5000 kununua bundle naambiwa salio halitoshi, kuangalia salio nakuta 4847 sasa nauliza hiyo nyingine imeenda wapi? mbona sijawaambia wanikopeshe?
 
Hili tatizo limekuwa sugu sana
TCRA tazamen huu mtandao
 
Jana kulikuwa na salio TSh 210 baada ya kuona thread hii nikaona ngoja nione kwangu kama bado ipo ila cha kushangaza😢😢 kuna 0.00 na laini yao ipo kwenye kisimu kidogo sijui watasema sikuzima data.?
 
Inatokea sana...

Wanakukata kwa njia za kukuletea sms kwenye mambo ambayo hujawahi ku-subscribe...

Cc: mahondaw
 
Na wamepandisha bei za vifurushi wakifikiri wote ni wakina Bakhresa au DAB.
Yaani 2000, nawekewa 5MB, na hata TIGO nao wameiga toka voda nahisi.
Hawa wamebaki kuwa wanyonyaji wakubwa.
 
Inatokea sana...

Wanakukata kwa njia za kukuletea sms kwenye mambo ambayo hujawahi ku-subscribe...

Cc: mahondaw
Siyo kwa ajili ya SMS. Hata bila ya kuletewa SMS fedha zinapungua. Ni tatizo sugu. Ukiweka fedha bila kujiunga baada ya muda utaambiwa hakuna salio au unaambiwa halitoshi. Uzime data haisaidii. Na hata ukiwa na bando jingine active haisaidii.
 
Hao jamaaa hawafai wanafagia tuu kila hela inayoonekana ya vocha wanaiba hadi aibu
 
you might be true my friend!

Several time imenitokea, data ya bundle yangu imeisha, nanunua vocha nikiweka (NAZIMA DATA KABLA KUWEKA), nikitaka kuunga bundle naambiwa salio halitoshi! Mara nyingi sana imenitokea hii

Mfano jana tu!
bundle limeisha, nikazima data nikaweka vocha ya 5000 kununua bundle naambiwa salio halitoshi, kuangalia salio nakuta 4847 sasa nauliza hiyo nyingine imeenda wapi? mbona sijawaambia wanikopeshe?
Aisee same to me, mpaka naamua niingize ela M- pesa , nowadays najiunga moja kwa moja kupitia mpesa
 
watakwambia haukuzima data,,,,
voda wapuuzi sana na sms zao mambo vipi, ofa kwa ajili yako ,pata mb 70 kwa 500 tu,,vigezo na masharti kuzingatiwa
mambo vipi my foot..............
Hahahahaha

Wanauzi kama nini??
 
Wadau habari? ukweli ni kwamba, hawa vodacom, ukiingiza salio bila kujiunga na kifurushi basi hilo salio wanalipiga juu kwa juu. imenitokea mara nyingi. naweka salio ili niweze kutumia simu banking bila hata kutumia baada ya mda naona salio hamna. kwanini ninunue vocha kwenu halafu mniibie salio bila hata kutumia?
Na wanaiba kweli,jaribu kuweka labda sh 300 usipoitumia baada ya masaa 24 huikuti,wameshaiba tayari au unakuta washaipunguza imebaki sh 200.
Hawa jamaa nao ni mafisadi,serikali iwachunguze
 
Hivi mitandao yao haina huduma ya kusisitisha ili lisitume salio badala ya MB ikiwa data ipo wazi?

Huku tunainjoy kabisa.

Ukiwa Huna MB na salio limo haliendi kabisa.
 
Hakikisha umezima data, kama hauna kifurushi cha data

Back
Top Bottom