Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
Kwanini hawafanyi kama wanavyofanya CCM, kuwaandaa vijana wao wa jinsia zote, na kuwapa fursa na nafasi tofauti tofauti za uongozi hata baada ya kuhudumu katika jumuiya za urika wao wa awali?
Maskini ya Mungu, vijana wengi kwa mfano upinzani, wanaishia tu kwenye idara zao za nyakati za ujana wao ndani ya vyama vyao, halafu baada ya hapo hawaonekani tena na wala hawapewi nafasi wala fursa tena za uongozi kwenye ngazi nyingine za juu.
Mbaya zaidi jinsia, hususani ya kike haizingatiwi kabisa kupatiwa fursa za uongozi ndani ya vyama vya siasa hadi inatia huruma.
Katika baadhi ya vyama siasa kwa mfano, waliowahi kua vijana zamani wameanza kuzira, kususa kimya kimya na kujitenga na shughuli za kichama kabisaa, kwasababu hakuna matumaini tena ya kupata nafasi au fursa huko juu katika vyama.
Kuna vyama vya siasa humu nchini, tangu kuanzishwa kwake miaka zaidi ya 20 iliyopita, mwenyekiti wake na viongozi wengine waandamizi ni wale wale na hawana dalili za kuwaandaa au kuachia wengine kwa utaratibu wa succession plans, wala hawana nia ya kuwapa fursa na nafasi za uongozi wa juu kwa wanawake..
Friends, ladies and gentlemen, unadhani changamoto ni nini hasa, hata succession plans isiwe na umuhimu ndani ya vyama vya siasa na kukumbatia uhafidhina?🐒
Mungu Ibariki Tanzania