Kwanini vyama vya siasa nchini havina succesion plan kutoka rika moja hadi rika jingine?

Kwanini vyama vya siasa nchini havina succesion plan kutoka rika moja hadi rika jingine?

Ni vitega uchumi vya watu kwa ajili ya kuwapatia pesa kuendeshea maisha yao.
unakuta kijana mdogo tu upinzani, eti kastaafu siasa, kumbe maskini ya Mungu hakuna matumaini ya fursa wala nafasi anaweza kupata nafasi ya uongozi kwenye chama chake kwasabb viongozi wao ni wa maisha 🐒
 
Kwanini hawafanyi kama wanavyofanya CCM, kuwaandaa vijana wao wa jinsia zote, na kuwapa fursa na nafasi tofauti tofauti za uongozi hata baada ya kuhudumu katika jumuiya za urika wao wa awali?

Maskini ya Mungu,
vijana wengi kwa mfano upinzani, wanaishia tu kwenye idara zao za nyakati za ujana wao ndani ya vyama vyao, halafu baada ya hapo hawaonekani tena na wala hawapewi nafasi wala fursa tena za uongozi kwenye ngazi nyingine za juu...

Mbaya zaidi jinsia, hususani ya kike haizingatiwi kabisa kupatiwa fursa za uongozi ndani ya vyama vya siasa hadi inatia huruma..

Katika baadhi ya vyama siasa kwa mfano, waliowahi kua vijana zamani wameanza kuzira, kususa kimya kimya na kujitenga na shughuli za kichama kabisaa, kwasababu hakuna matumaini tena ya kupata nafasi au fursa huko juu katika vyama.


Kuna vyama vya siasa humu nchini, tangu kuanzishwa kwake miaka zaidi ya 20 iliyopita, mwenyekiti wake na viongozi wengine waandamizi ni wale wale na hawana dalili za kuwaandaa au kuachia wengine kwa utaratibu wa succession plans, wala hawana nia ya kuwapa fursa na nafasi za uongozi wa juu kwa wanawake..

Friends, ladies and gentlemen,
unadhani changamoto ni nini hasa, hata succession plans isiwe na umuhimu ndani ya vyama vya siasa na kukumbatia uhafidhina?🐒

Mungu Ibariki Tanzania
We unaongeza ushabiki bila tafiti za kutosha! Ubunge sio muhimu? Angalia vijana walivyokuwa Bungeni mwaka 2005-2020,Wazee wabungecwengi walikuwa SM mpaka wanasinzia!Anaambiwa atoe kero za Jimbo lake,anaishia kucopy na kupaste eti kama alivyosema kimwakaleli!
 
Pumbavu sana wewe, CCM siyo chama cha siasa? CCM ina succession plan au ina heritage plan? Usidange watanzania asilani, kilichopo huko ni kwamba kigogo kabla hajakata ringi ashahakikisha watoto wake na ndugu zake wachache wapo katika hatua gani kutawala nchi? Unamwona Mwigilu kila siku akimpost mtoto wake ambaye pia sasa na mtoto ameanza kutoa misaada at his tender age lkn wanaopokea hiyo misaada ni wazee wenye umri zaidi ya Mwigulu? Hiyo ndo kurithi siyo succession. Understand? Lakini watanzaia wanaona hayo yote, wanaona ni kinyume na utaratibu siku ya siku majibu yataoatikana.
Muerevu mbona umekurupuka na mihemko tu? Relax na ujieleze taratibu tu wadau watakuelewa vizuri zaidi...

sasa hiyo succession plans ya huyo uliemtaja ni kinyume na utaratibu wa nani?

kama wewe ni mkulima na unataka kumuandaa mwanao awe mkulima, mvuvi, mfugaji, mfanyabiashara au msaanii kuna ubaya gani gentleman?

Yaani unapata mihemko juu ya namna familia ingine inavyofanya succession plans kwa watoto wa rika zao mbalimbali? alaa?

si na wewe uandae wanao? sijui watakua watu wa mihemko au kulalamika tu?🐒
 
We unaongeza ushabiki bila tafiti za kutosha! Ubunge sio muhimu? Angalia vijana walivyokuwa Bungeni mwaka 2005-2020,Wazee wabungecwengi walikuwa SM mpaka wanasinzia!Anaambiwa atoe kero za Jimbo lake,anaishia kucopy na kupaste eti kama alivyosema kimwakaleli!
nazungumzia succession plans gentleman ndani ya vyama vya siasa..

vipi kuhusu vyama visivyokua na wabunge wanayo?🐒
 
Kitu gani kimekukwaza hapo ndugu?
nimeona tu ukomo wa mawazo mapya na fikra mbdala, mwanzo sana wa hoja hii muhimu mno ya succession plans ndani ya vyama vya siasa 🐒
 
Kwa hiyo wewe na Mwashambwa ndio planners wa SM!
hii issue inahusu succession plans ndani ya taasisi za siasa, sio kwa ajili sijui ya fulani na fulani kwa majina..


huu ni mpango muhimu sana na wa maana mno kwa mustakabali mwema wa usitawi wa Demokrasia na uongozi ndani ya vyama vya siasa na baadae uongozi wa nchi 🐒
 
hii issue inahusu succession plans ndani ya taasisi za siasa, sio kwa ajili sijui ya fulani na fulani kwa majina..


huu ni mpango muhimu sana na wa maana mno kwa mustakabali mwema wa usitawi wa Demokrasia na uongozi ndani ya vyama vya siasa na baadae uongozi wa nchi 🐒
Wazo zuri Anza kwanzo huko kwenu SM,tutawaiga, maana nyie ndio mlioshika Dola hata mkiandamana!
 
Huko Vyuoni kila Mwanafunzi anaamini kuwa CCM ndio tiketi yakuajiriwa/kuteuliwa baada ya kumaliza masomo
na ndio matumaini na ndoto ya waTanzania wote zilivyo, hasa chini ya serikali sikivu ya CCM chini ya kiongozi madhubuti na makini sana, Dr.Samia Suluhu Hassan, na wengi sana wamefanikiwa na mamilioni bado wanaendelea kufanikiwa 🐒
 
nadhani ccm iko wazi sana kwenye mambo ya succession plans, mathalani, Mwenyekiti wa CCM Taifa, katibu mkuu wa CCM Taifa, Muenezi Taifa, katibu mkuu msaidizi, mawaziri, wakuu wa wilaya na mikoa wote hao ni matokeo ya succession plans ya chama na serikali...

sina mfano kwa upande wa upinzani kwasababu hakuna kabisa, wamezira kabisa wamekua kama wastaafu tu 🐒
Wazee wa weka ndani bila sababu,huku kila uchwao ,madudu ya upigaji yanatolewa,wote hao ni SM kwa SM!
Succession plan ipo. Nenda Singida, nenda Tanga, Nenda Arusha , Pwani na kwingineko...vyama vimefanya hivyo. Ingawa Kuna baadhi ya vyama baadhi ya nafasi muhimu havitaki hiyo kitu ya succession plan!!
Hata Mbeya Mara nk!
 
Back
Top Bottom