Kenya 2022 Kwanini vyombo vya habari nchini Kenya vimeacha kuonesha matokeo ya urais?

Kenya 2022 Kwanini vyombo vya habari nchini Kenya vimeacha kuonesha matokeo ya urais?

Kenya 2022 General Election
Sijui kuhusu kupinduliwa....lakini binafsi naona toka mwanzo ingetakiwa kufanya kama wanavyofanya sasa.

hauwezi kujumlisha kura kabla ya kuzihakiki physically. media zilikuwa zinajumlisha 34A za online (nipo tayari kusahihishwa)
Physical kivipi mkuu?;wakati zile zilikua scanned from the originals.

Matokeo hayatangazwi sababu sahivi IEBC inatoa matokeo ya Jimbo (Form 34 C) hivyo imerahisisha maana fomu zipo 200+ tofauti na Form 34A ambazo zipo 48k
 
Ukiona hivyo yanapinduliwa hayo.
Toka juzi.
Ila ntashangaa sana Raila akishinda.
Huyo mzee kachoka wamwonee huruma tu wasimpe apumzike.
Kwa hiyo wamarekani ambao kutwa mwawapigia mfano ni wapuuzi?
 
Toka juzi vyombo vya habari nchini Kenya viliweza kurusha matokeo ya urais. Leo asubuhi wameacha kuonyesha. Hii ni kwa vyombo vyote, Kilichobaki tu ni kuonyesha matokeo ya kila Kaunti. Nashindwa kuelewa shida nini maana tumekuwa tunafuatilia kwa urahisi.

Sasa, Shida ni nini?

Ni kweli mtandao umekatika?

Wamegundua kuna tatizo litajitokeza?

Wamenyimwa access ya 34A au?

au mimi ndiye mwenye haraka labda wataendelea baadae?
Form 34A unaweza access hata ukiwa hapo kwako Vingunguti bora uko na internet. Sisi sio nchi ya kiimla na ya ukandamizaji Kama hiyo yenu
 
Wewe usitudanganye,Tume imepiga stop TV stations zote kutoa matokeo
Unataka watoe matokeo gani wakati kufikia jana saa kumi jioni 99% of forms 34A were already uploaded? Kinachofanyika sasa ni verification na mfano ushapewa hapo juu in post #10
 
Sijui kuhusu kupinduliwa....lakini binafsi naona toka mwanzo ingetakiwa kufanya kama wanavyofanya sasa.

hauwezi kujumlisha kura kabla ya kuzihakiki physically. media zilikuwa zinajumlisha 34A za online (nipo tayari kusahihishwa)
Media walifanya vizuri sana kwani wamewapa wananchi picha ya mchuano. Kama ulivyosema; uko sahihi. Tume ya uchaguzi ilipokea fomu kutoka kila kituo na ikaziweka kwenye mtandao bila kuzihakiki. Hivyo media ilikuwa inatoa mahesabu ya fomu ambazo hazijahakikiwa. Wanachofanya sasa hivi ni kuwa tume ndiyo imeanza kuhakiki na kuhesabu. Kilichofanya media isitishe mahesabu ni kuwa huu uchaguzi uko tight mno mno kiasi amabcho hata kuta moja inaweza kubadili matokeo yote hivyo media wanaona pengine kunaweza kukatokea baadhi ya fomu chache zenye hitilafu.
 
Bado hamjamaliza hilo timbwili...tayari umeshaanza mdomo.
Ngoja muanze kukatana vichwa ndio utajua Afrika ni moja.
Hilo ndio ombi la kila kila mtanzania kwenye hili jukwaa. Unashangaa kwa nini vyombo havitoi matokeo wakati kwenu hilo litabakia kuwa ndoto
 
Form 34A unaweza access hata ukiwa hapo kwako Vingunguti bora uko na internet. Sisi sio nchi ya kiimla na ya ukandamizaji Kama hiyo yenu

Bwege wewe! Nchi gani ni ya kiimla!
 
lakini naona haija serve the purpose....maana mpaka jana saa saba usiku kila chombo cha habari kilikuwa na idadi tofauti. Naelewa mwenye mamlaka ya kutangaza mshindi ni IEBC, wangeviacha vyombo vya habari viendelee kuonyesha data zilipofikia.

kwasasa hatujui ni nini kinaendelea.

udanganyifu gani The Boss ?
Kama umeshasema walikuwa wanaleta matokeo tofauti, tuendelee kuwaamini hao hao?
 
lakini naona haija serve the purpose....maana mpaka jana saa saba usiku kila chombo cha habari kilikuwa na idadi tofauti. Naelewa mwenye mamlaka ya kutangaza mshindi ni IEBC, wangeviacha vyombo vya habari viendelee kuonyesha data zilipofikia.

kwasasa hatujui ni nini kinaendelea.

udanganyifu gani The Boss ?
Ndugu hizi vitu hupikwa hata huko marekani humuweka wanaemtaka! Demokrasia ni danganya toto maana demokrasia inamatobotobo Sana ngumu kuyafunika!..
Kuwapa uhuru huo ni kujitia dosari penye asali..😁
 
Kwa mujibu wa tovuti ya National online, mpaka muda huu naandika hapa matokeo waliyoyatoa wameyapata kutoka kwenye vituo vya kupigia kura 41000+ (ni wastani wa 90%) kati ya vituo ya vituo vyote 46000+, hivyo kuna karibu vituo 5000 bado matokeo yake hayajawekwa na mtandao huo. Hivyo hesabu ya kura za mtandao huo huenda zinawakilisha wastani wa 90% ya matokeo yote.
 
Hakuna TV iliyokuwaq inatoa matokeo, walichokuwa wanafanya ni kuoneshwa kura zilizojumlishwa! Nationa online inaonesha jumla ya kura halali zilizoenda kwa wagombea ni 13,427,287. Bila kujumlisha kura zilizoharibika ambazo pia ni maelfu kadhaa. Jumla ya waliopiga kura ni 14,164,561. Ukitoa kura halali unabaki na 737,274. Hii idadi inawakilisha kwa kiasi kikubwa kura ZILIZOHARIBIKA na kura chache zilitokana na manual registration of few voters. Kwa hiyo kura za kujumlisha ni kama zimekwisha! (almost over ).
Haya ni maneno matupu yasiyokuwa na chanzo cha uhakika zaidi ya kutuletea zile numbers za NATION hapa ambazo hazina maana sana.
Chebukati ndiyo kwanza anatangaza matokeo,naona wengine wanakimbilia kuleta screenshot za Reuters ambayo ni yale yale tu sawa na NATION.Hapa msema kweli ni Chebukati peke yake,vinginevyo tuendelee kupiga blah blah tukisukuma muda kungonjea matokeo rasmi.
 
Hapa Afrika Demokrasia ya maana iko Tanzania tu. Ukishapitishwa na chama Tawala tayari we ni Rais hata kabla ya uchaguzi. Uchaguzi ukifanyika matokeo ni simple majority MTU anatangazwa ! Demokrasia ni ngumu jamani hata wamarekani imewashinda. Ingekuwa rahisi basI HILARY CLINTON angekuwa Rais wa Marekani.
 
Hilo ndio ombi la kila kila mtanzania kwenye hili jukwaa. Unashangaa kwa nini vyombo havitoi matokeo wakati kwenu hilo litabakia kuwa ndoto

Hamna Mtanzania anaeombea fujo Kenya . Fujo yoyote Kenya , Tanzania itaadhirika kiuchumi pia nitashindwa kupeleka vitunguu Nyamakima.
 
Hilo ndio ombi la kila kila mtanzania kwenye hili jukwaa. Unashangaa kwa nini vyombo havitoi matokeo wakati kwenu hilo litabakia kuwa ndoto

ujinga wako ni special.

kwahiyo kila upuuzi unaotokea huko ni lazima ufananishe na TZ kwanza??kama una afadhali basi ni halali.
 
ujinga wako ni special.

kwahiyo kila upuuzi unaotokea huko ni lazima ufananishe na TZ kwanza??kama una afadhali basi ni halali.
It shows our democratic space. But you can't understand coz you don't understand
 
Back
Top Bottom