Wahindi wanajua sana kuwatumikisha wafanyakazi za ndani hasa wanawake. Pamoja na kwamba wanawapa mshahara sawa na wa kima cha chini cha serikali. Pia mfanya kazi hua anahudumu ndani ya muda wa kisheria wa muajiriwa.
Ila wahindi wanahakikisha kazi zinqfanyika kwelikweli. Yaani wanapata thamani halisi ya mishahara wanayotoa
Tatizo la waswahili wanataka mambo meengi sana kwa mfanyakazi. Mara asiwe na mtoto, asiwe mbea, asiwe na simu, asiwe na ndugu wala rafiki japo haingilii kazi zake, asiwe, asiwe asiwe......!!!! Marufuku kibao
Mshara sasa ndio kasheshe. Na kwa vile anakaa hapo nyumbani basi kazi anamaliza saa sita usiku na anatakiwa aamke tena saa kumi na moja alfajiri!!!
Kibaya zaidi ajira za hawa wadada wa kazi zipo mikononi mwa kina mama na wao ndio wanongoza kuwa mistreat! Mwnaume ukitaka kuingilia ili atendewe haki utaambiwa ni demu wako au unamtaka!!!