Kwanini wachawi hutupia watu majini?

Kwanini wachawi hutupia watu majini?

Sijaelewa swali lako.
Mnasema kwamba kwenye uchawi majini ndio hutumika kwa maana ya majini hutumwa ili kufanikisha yaliyokusudiwa na mchawi, ndio mimi nauliza kwamba unadhani hayo majini hupenda kutumika au kutumwa hivyo?
 
Malaika mkuu ni cheo sio kitu cha kuzaliwa nacho
Mimi sizungumzii cheo chake bali nazungumzia asili yake, hata binaadamu tuna kuna wenye vyeo vya urais au ufalme ila asili ni binaadamu. Sasa sijaelewa Ibilisi asili yake ni malaika au alikuwa na cheo tu cha malaika mkuu ila hakuwa malaika?
 
Mnasema kwamba kwenye uchawi majini ndio hutumika kwa maana ya majini hutumwa ili kufanikisha yaliyokusudiwa na mchawi, ndio mimi nauliza kwamba unadhani hayo majini hupenda kutumika au kutumwa hivyo?
Hakuna sehemu niliyosema au tunayosema majini hutumwa sababu hakuna anae weza kuyatuma majini bali kinyume chake ndiyo ukweli,Wachawi wanawategemea majini,hata hizi taarifa wapatazo wachawi huzipata kupitia majini.

Mwanadamu hana uwezo wa kumtuma Jini wala haikuwahi kuwezekana wala hakuna anae fuga majini wala haitatokea wenye kusema hayo hawawajui majini.
 
Ok tuanze kwanza na kujua jini ni nini au ni kiumbe gani?
 
Ok tuanze kwanza na kujua jini ni nini au ni kiumbe gani?
Jini ni kiumbe alie umbwa malighafi moto,alianza kuumbwa kabla ya mwanadamu. Amepewa uwezo wa kujibadili katika maumbile tofauti tofauti kama vile umbile la nyoka mweusi au mbwa mweusi au punda mweusi, na amepewa uwezo wa kuingia katika mwili wa mwanadamu.

Kadhalika ni ngumu kumuona jini katika umbile lake la asili.

Tuendelee...
 
Sasa inakuaje kiumbe huyo(jini) aje kuhusika na masuala ya uchawi?
 
Sasa inakuaje kiumbe huyo(jini) aje kuhusika na masuala ya uchawi?
Kihistoria uchawi upo wa aina mbili nao ni :

1. Uchawi walio kuja nao Malaika wawili Haruti na Marut.

2. Uchawi walio nao majini, uchawi wa majini ni ule wakuua,kuroga na kuwadhuru watu. Huu ulionekana sana kipindi cha nabii Suleyman.
 
Ndio nimetaka kujua uhusika wa majini kwenye uchawi ni upi? Na huo uchawi waliyokuja nao malaika ndio upi?
 
Ndio nimetaka kujua uhusika wa majini kwenye uchawi ni upi? Na huo uchawi waliyokuja nao malaika ndio upi?
Uhusika wa majini katika uchawi nimeshakueleza hapi juu ya kuwa wao ndiyo walikuwa wanawafundisha wanadamu mambo ya uchawi.

Uchawi walio kuja nao Malaika wawili na kuwafundisha Wanadamu ila kwa kuwapa angalizo kabla ya kuwafundisha ni uchawi wakuwafarakanisha Mume na mke.
 
Asante
Uchawi ni kaliba yenye ujuzi tofauti tofauti
Kuna uchawi wa vitabu
Kuna uchawi wa tunguli
Kuna uchawi wa mapepo
Kuna uchawi wa majini nknk
Maranyingi kila aina ya uchawi una eneo lake....kwa mfano uchawi wa mawajini maranyingi hupatikana maeneo ya pwani
Kumbuka kila mchawi ana ujuzi wake na hawaingiliani kabisa., ni wale makonkodi pekee ndio wanaweza kuhodhi juzi kadhaa
Mkuu hivi kwa mfano uchawi wa kutupiwa majini unaweza kuteguliwa na mganga au mpaka mchawi mwenyewe alietupia hayo majini..

Msaada! plz maana kuna mtu wangu wa karibu anasumbuliwa na uchawi wa aina hii kutokana na wataalamu wanavyoona kwenye screen zao na ni miezi kadhaa sasa inaelekea na bado hayo mapepo hayajatoka yote.
 
Uhusika wa majini katika uchawi nimeshakueleza hapi juu ya kuwa wao ndiyo walikuwa wanawafundisha wanadamu mambo ya uchawi.

Uchawi walio kuja nao Malaika wawili na kuwafundisha Wanadamu ila kwa kuwapa angalizo kabla ya kuwafundisha ni uchawi wakuwafarakanisha Mume na mke.
Twende taratibu.

Ulisema kwamba wachawi wanawategemea majini kwenye huo uchawi wao kwa maana ili uchawi uweze kulete athari au kufanyika ni lazima jini ndio ahusike, sasa ndio nikataka kujua kwamba kwanini majini wajihusishe na hicho kinachoitwa uchawi yani kwamba wawafundishe watu uchawi na huo uchawi wenyewe ili uweze kuleta matokeo basi ni majini hao hao ndio uhusika(hutumika) ndio maana nauliza kinachowafanya wajihusishe na huo uchawi ni nini?

Na huo uchawi waliyofundisha malaika pia majini uhusika pia(hutumika) au huko hawahusiki?
 
Mkuu hivi kwa mfano uchawi wa kutupiwa majini unaweza kuteguliwa na mganga au mpaka mchawi mwenyewe alietupia hayo majini..

Msaada! plz maana kuna mtu wangu wa karibu anasumbuliwa na uchawi wa aina hii kutokana na wataalamu wanavyoona kwenye screen zao na ni miezi kadhaa sasa inaelekea na bado hayo mapepo hayajatoka yote.
Majini ya kutupiwa hutolewa kwa mganga lakini pia hata bila mganga zipo dawa hutumika kufukuza au kuondosha majini mwilini au hata kwenye nyumba.

Kwa uelewa wangu naelewa hivyo.
 
Uchawi ni uwezo wa binadamu kufanya matukio au mambo ambayo yako nuu ya uwezo wa kibinadamu kwa kutumia nguvu za ziada ambazo zinatolewa ama huyo mtu anawezeshwa na shetani ama mawakala wake.

Uwezo huo ni kama kutembea usiku ama mchana bila kuonwa na binadamu wenzake, kuingia kwenye nyumba bila ufunguo, uwezo wa kumletea binadamu mwingine ama kumtengenezea madhara kama ajali, ugonjwa, kifo ama ulemavu na mambo kama hayo.

Sasa vitu hivyo ni fikra tu kwani kwa uhalisia havipo na havijawahi kuwepo na wala uwezo kama huo haupo na haujawahi kuwepo.

Kukuta mtu ana mawazo kama hayo basi unajua kabisa akili hana.
Watu walipogundua kutengeneza umeme .. ule ulikua uchawi au sio uchawi au kurushamawimbi ilikua ni nini

Sent from my JSN-L21 using JamiiForums mobile app
 
Sijasema ya kuwa Adamu alikuwa malaika.

Swali langu la msingi ni kwa Ibilisi kuwa Malaika Mkuu. Hili linawezekana vipi ?
Nadhani nimekujibu kuwa hicho ni cheo sasa ukiniuliza inawezekana vipi kukipata hicho cheo hapo kwakweli sina jibu.. Je umenielewa sasa?
 
kutoka 7:22-25 hakuna neno uchawi instead of neno waganga ndo lipo
Je andiko lako ni kutoka biblia ya Tafasili ipi?

Chanzo changu ni BHN
Ingia hapa uhakiki: Kutoka 7:22-25 Lakini wachawi wa Misri kwa kutumia uchawi wao wakafanya vivyo hivyo. Kwa hiyo moyo wa Farao ukabaki kuwa mgumu, naye hakuwasikiliza Mose na Aroni; ikawa kama Mwenyezi-Mungu alivyokuwa amesema. Basi, | Biblia Habari Njema (BHN) | Pata programu ya bure ya Bibilia sasa hivi.

Mbona ww mwongo san jamaa angu
Kwanza kuwa mstaarabu, Jenga hoja, Pinga hoja kwa Hoja, Utaeleweka zaidi, Pili hebu ithibitishie Jamii pasi na shaka huo uongo wangu.

Back to Topic, Kwenye biblia ni sehemu nyingi neno uchawi limetajwa.

Hakiki mwenyewe hii mifano zaidi toka kwenye biblia.

#1. Nahumu-3: Kiswahili Biblia - Agano la kale
1643169925247.png

#2. Matendo ya Mitume-8: Kiswahili Biblia -
1643169962381.png

#3. Isaiah-47: Kiswahili Biblia - Agano la kale
1643170010342.png

#4. Mika-5: Kiswahili Biblia - Agano la kale
1643170049049.png

#5.
1643170095129.png

Ndugu mosses son kuwa na amani, Uwe na siku Njema.
 
Nadhani nimekujibu kuwa hicho ni cheo sasa ukiniuliza inawezekana vipi kukipata hicho cheo hapo kwakweli sina jibu.. Je umenielewa sasa?
Yaani swali langu hujalijibu kwa maana ya kuwa Jini anawezaje kuwa Malaika tena akawa mkuu ?

Au hujui kama Ibilisi ni katika majini ? Malaika ni jinsi kama ilivyo mwanadamu au Jini ?
 
Back
Top Bottom