Kwanini wafanyabiashara wanakwepa kusajili stoo zao? Taarifa zinasema wamejaza mali za magendo baada ya kuziingiza nchini isivyo halali

Kwanini wafanyabiashara wanakwepa kusajili stoo zao? Taarifa zinasema wamejaza mali za magendo baada ya kuziingiza nchini isivyo halali

Wafanyabiashara wengi wanaingiza mizigo kwa njia ya magendo, wanazitunza stoo. Wanaweza kupitishia bandarini, njia zisizo rasmi za mipakani, au kwa majahazi. Hawalipi Kodi.

Sasa serikali imeamua kusajili stoo wanazotunzia ili waweze kujua zilipo, wakague na waonyeshwe risiti za jinsi mzigo ulivyoingia, kama wewe umeingiza mzigo kihalali, kwa nini uone kero Afisa wa serikali kuja kuikagua?

Serikali isirudi nyuma katika hilo. Tunaona wamachinga Wana mzigo wanauza, kumbe wanatoa katika stoo ya tajiri, na tajiri anakuwa kauingiza kimagendo.

Kila mtanzania alipe Kodi, tunataka maendeleo, yatakuja vipi bila Kodi?

Nawashauri TRA hiyo kariakoo waiweke katika maeneo madogo madogo ya kiutawala. Iwe special zone. Wanauza bila risiti, waachwe tu? Hapana.

Huyo kiongozi wao serikali im-pin down kwa uhujumu uchumi, na biashara zake zikione Cha moto
Acha mambo yako wewe ya kitoto. Wapi magendo yanaingia TRA hawapo? Tanzania hii unaweza kuingiza mzigo contena TRA wasijue au kuchukua posho. Kwa taarifa yako ukiona mtu anaingiza magendo hapo ujue kuna fungu wanapewa TRA na polisi uwezi kukwepa hawa watu lazima uwe salama kwanza ndo uingize mzigo. Sasa hapo mwenye makosa ni nani kati ya TRA na mfanyabiashara? Shida TRA ni waonezi sana kutishia kuwafilisi watu na kuwapa madeni ambayo sio ya kweli. Wao wamesema hawataki kukagua store ila wanataka Kodi ya store. Mzigo ambao upo store na wenyewe uwe na kodi kama uliopo dukani.
 
Kwani wao ulipaji wa kodi ni tofauti na wafanyabiashara wengine?inshu sio utaratibu hawataki kutumia EFD,kwani wengi hawapendi kuandika thamani halisi ya mauzo,na ndio maana kariakoo kuna watumishi wa TRA wao ni kufuatilia wateja,wanaokuwa wamenunua bidhaa,na unakuta mtu ana tv ya thamani ya laki 6,ila risiti aliyonayo imeandikwa laki 2!
Na usajiri wa store ndio umewavuluga mnooo!!
Hiyo mbinu tunafanya sana asee,, 😂 😂
 
Huwezi kudai kodi kwa kubembeleza,, utavuna mabua
Hatusemi wabembeleze, tunasema warekebishe sheria zinazoua biashara na kukosesha serikali mapato, matoke yake zinachagiza rushwa kwa akina boni wanaojenga maghorofa huko
 
Back
Top Bottom