Johnny Sack
JF-Expert Member
- Jan 21, 2017
- 8,984
- 19,288
nimekuwa nikifuatilia mtandaoni na mtaani, Rais Samia akikutana na wapinzani kujadili mambo ya siasa au mambo mengine, wafuasi wa Magufuli wamekuwa wakichukia na kutukana sana
Ilianzia Samia alipokutana na Tundu Lissu alipoenda Ubelgiji, wafuasi wa Magufuli walilaumu sana na kudai Samia anakutana na wasaliti wa nchi, kwanza anasafiri hovyo wakati nchi ina matatizo
Pia mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe alipoachiwa kwenye ile kesi iliyokuwa ikimkabili, wafuasi wa Magufuli walifura sana na wakashindwa kuficha hasira na chuki zao, wakasema Rais anatumia vibaya mamlaka yake kusamehe wahalifu wenye makosa makubwa kama ya ugaidi, wengine wakasema wanataka Sabaya aachiwe pia sababu Mbowe kaachiwa
Juzi pia kwenye mkutano waliofanya na Chadema Ikulu, wakawa wanaponda tena, mara hii wakasema Chadema wamenunuliwa wanaenda Ikulu kila siku, hakuna kuikosoa Serikali tena...
Hawa watu wanaona kama Chadema hawaikosoi Serikali kwa nguvu na wanataka waone Chadema ikiwa aggresive kwa Samia sana, lakini hawa mbona walikuwa wanawapongeza wapinzani kama akina Mrema waliokuwa dam dam na CCM, waliona Upinzani kutoikosoa Serikali ni uzalendo, lakini sasa hivi wanalalamika Chadema kutoikosoa Serikali (japokuwa Chadema wamekuwa wakiikosoa anyway)
Jana kumekuwa na taarifa ya Samia kumlipa mafao yake Tundu Lissu, ambalo ni jambo jema sana ukizingatia aliyopitia Lissu, wafuasi wa Magufuli na hili imewauma sana hadi nimeshangaa, wanaona Samia ni kama anachezea fedha za umma kumlipa mb unge stahiki zake?
Hawa wafuasi ni kwa nini hawapendi kuona kuna haki nchini? kwa nini wana hamu ya kuona watu wanauawa na kuswekwa rumande tu kila mara? hawa watu wana asili ya tanzania kweli? Hawa watu wana hamu ya kunywa damu za watu muda wote?