OSEFUKANY
JF-Expert Member
- Jan 16, 2011
- 2,437
- 3,896
La Hasha. Kwa mfano hapa Tz, ukienda Mtwara eneo la Naliendele utauziwa (sio kupewa bure)konokono na ukienda Denmark eneo la Slagelse unakula konokono na kaa (Crabs) na ni chakula cha bei mbaya. Je, hao wamekosa kitu gani halafu wewe unaviita ni takataka? Ukija huku kwetu Umasaini ndani huku, samaki hata kumtazama tu ni shida -hawamtaki kabisa ni takataka kwao - wanatema hata mate wakimwona halafu ww unamwona samaki ni chakula bora? Ubora au Uzuri wa chakula upo kichwani mwako. Sisi wenzio tunakula ww kalaghabaho.Kula takataka kama hizo inaashiria huna options za vyakula vinavyofaa......kwa akili ya kawaida unaanzaje kula hivyo vitu ikiwa umezungukwa na samaki, kuku, ngo'mbe, mbuzi........ukiona sehemu vitu vya namna hiyo vinaliwa lazima kuna uhaba mkubwa wa vitoweo.