Ni kweli kwenye Quran kuna kifungu kinachomruhusu muislam kujitoa muhanga na endapo atafanya hivyo atapewa mabikra 72 akifika ahera? Hii ni kweli au stori tu za mitaani?.
Kikifanywa kwa uzuri kwa kile mtu alichoelekezwa hupatiwa zawadi kulingana na uzuri alioufanya. Falsafa hii kwa binadamu inafanya kazi vilevile. Lakini muasisi ni Mungu.
Hakika kwa upande wa Mungu, mja akiyashika ya Mungu na kubakia kwake atalipwa kwa uzuri wa kile alichojitahidi. Na Mungu ametupatia haya maumbile na akayajaza kupenda nini.
Kwa wanaume tumeumbiwa kupenda mengi na mojawapo ni wanawake kwa sababu ndiyo maumbile tuliyopewa. Peponi kuna neema nyingi na kwa mwanamume ni kuozeshwa wanawake.
Lakini Mungu hapendezeshwi na kuua. Ukitoa uhai 1 ni sawa umetoa uhai wa watu wote duniani. Mtoto wa Nabii Adam A.S aliemuua nduguye kwa sababu yeye ndiye muasisi wa kuua basi kwa kila binadamu atakaefanya dhuluma ya kuua asilimia ya madhambi ya uuaji naye yanamfikia kwa sababu yeye ndiye muasisi wa hiyo dhambi.
Ndiyo maana ukiua una laana ya Mungu, kwa sababu kuua ni sawasawa na kuvunja jengo alilolijenga Mungu. Kwa sababu binadamu ni wa Mungu halafu wewe unamuua.
Kuua kuliko ruhusiwa ni kuua kwa haki, nako ni kupi? Mfano vitani, umevamiwa na majambazi wenye silaha pengine una nyenzo za kupambana nao kwenye kupambana ukamuua hapo hauna dhambi na mfano wa namna hiyo!
Na ukimuua wewe ni peponi yeye ni motoni. Na ukiuliwa wewe ni peponi na yeye ni motoni. Kwa sababu wewe unaipigania haki kwa kuondoa udhalimu na yeye anaivunja haki kwa kuutangaza udhalimu. Ndivyo mafundisho ya Uislam.
Na Mungu ndiye mjuzi zaidi.