Phdum
JF-Expert Member
- Apr 15, 2019
- 1,322
- 3,278
Kuna mila na imani nyingi saana potofu. Niliishi kwa wajita huko kijiji fulani karibu na kibara. Kuna siku nyoka mkubwa aina ya kifutu alionekana cha kushangaza badala ya watu kuanza kumshambulia walianza kukimbia kila mtu kutafuta njia yake.
Baadae wakaja na mfuko eti wanambembeleza aingie ndani ya mfuko wampeleke porini. Ikabidi niulize ndio naambiwa wanaamini huyo nyoka wakimuua ni mikosi na balaa itawaandama na sio kumua tu hata yeyote atakaye muona akiuwawa nae nuksi na mikosi itamuandama.
Lakini pia wengine wanasema huyo nyoka wanamsujudi kama sehemu ya mizimu yao. Nilibaki nacheka tu maana mimi ninachojua ukimuona nyoka ni kuwahiana tu kummaliza.
Je, huko kwenu vipi mkimwona nyoka mnapiga naye picha au mnawaita Maliasili.