Kwanini Wajita hawaui nyoka aina ya kifutu? Bado wanaamini katika nyoka hao?

Kwanini Wajita hawaui nyoka aina ya kifutu? Bado wanaamini katika nyoka hao?

Kwanini umuue sasa, ni bora umpeleke huko porini labda kama anahatarisha usalama wako na wanao.

Ninyi ndo ambao mnaua viumbe hovyo hovyo tu, ukiona sisimizi unakanyaga unaua, ukiona mjusi chap kwa haraka unampiga kiatu, umeona paka/mbwa jiwe au fimbo iko wapi upige uue. Yaani hata bila sababu yoyote basi tu ni ukatili.
 
Kila mahala pana mila, desturi na tamaduni zake mkuu..ukimshangaa mwingine na mila zake nae atakushangaa pia ww na mila zako hivyo kuna mambo mengine acha tu yabaki hivyo kila mtu aheshimu mila zake pamoja na za mwenzie.

wakerewe pia kuna koo ni mwiko kabisa kuua nyoka aina ya chatu. Wahaya nao pia kuna koo ni mwiko kuua aina fulani ya ndege...n.k
 
Inasemeksna huyu nyoka kumuona tu ni mikosi ama ishara ya msiba, nakumbuka nilimuona kwa mara ya kwanza na tulimuua ila huo mwaka baba yangu alifariki kulitokea mabalaa mengi pia kwenye familia sijawahi kukutana nae tena
 
Watu wa musoma wengi wanaabudu wanyama. Kuna kabila lingine kinaitwa WANYABASI wao wanamwabugu PUNDAMLIA kama Mungu wao
Sio watu Tu Hata baadhi ya mataifa na taasisi yanaabudu wanyama wanawekwa kama nembo sehemu mbalimbali mf:Nyoka yupo kwenye nembo za afya,,Hata Sisi tulimuweka kwenye mia tano ya noti,,Australia na kangaroo,,,Tz na twiga,,Ndege Eagle na taasisi ya CIA Marekani
 
Maeneo yetu ni sehemu tulizojenga nyumba zetu za kuishi ...kumbuka unapoenda kuchimba dhahabu unaenda sehemu zenye vichaka na mapori sehemu ambazo nyoka amekimbilia baada ya binadamu kuanzisha makazi sehemu ya walizokuwepo mwanzo

Sasa wameondoka wametuachia maeneo still bado tunawafuata maeneo waliyokimbilia. Ndiyo maana mzungu akaweka masharti marufuku kumuua nyoka au mnyama yoyote ndani ya mgodi
Aisee, umeeleza vizuri sana. Big up mkuu
 
Back
Top Bottom