Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa sababu watu wa Dar wakija mikoani kwa ndugu zao wanapokelewa vizuri.Kwanini watu Wa mikoani wanaenda Dar Kwa ndugu zao kama wanaona wananuniwa?
Ukiona umenuniwa ujuwe umekuja Kama zigo tu,umeshindwa kuja hata na Mahindi ya kuchemsha kutoka kwenu Bush lazima utanuniwa tu! Watu wamikowani mjiongoze Dar kila kitu ni pesa siku hizi!!
Mimi huwa na kuja na debe mbili za mchele na maharage alafu nakaa siku tatu tu, mbali na hilo muda wote huwa nakuwa busy hvyo huwa sigusi dona lenu,lakini bado hali ni mbaya.
Fikia lodge au guest house.
Nikija bara nimeenda kwetu nitafikia kwetu. Nikienda mkoa mwngne nitafikia lodge au hotelini.Halafu wewe ukija bara ndo ufikie kwangu kutaka mizawadi kedekede ?
Mimi ninadhani mara nyingi ukisafiri mkoa to mkoa lengo unaenda kusaka pesa. Kama ni issue ya kimatibabu hapo kwakweli kukaa hotelin au lodge haiwezekani itabidi tu ukae kwa rafiki au ndugu.Ikitokea huna pesa?
Kwakweli nakubaliana naye huwezi funga safari utoke ulikotoka uje eti ukae tu mwezi. Mtu mwingine hana hata issue eti kaja kupumzika at your own expenses.Watu wa dar hata awe na jumba kubwa ukifika tu lazma akuzingue,tuna ndugu mpaka BoT lakini ukifika anahis utakula mshahara wake wote,tena unakuwa na ratiba ya kukaa kwake wiki tu lakin ataona shida.
Hii ni nature,nahisi mungu kawafanya kuwa hvyo ili wapunguze kero,najua wangekuwa wakarimu wangekuwa wanapokea wageni wengi sana.