Kwanini Wakenya siyo wajanja kwenye hili?

Barbarosa

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2015
Posts
22,584
Reaction score
27,817
Pamoja na demokrasia yao nzuri na bora kabisa Duniani ambayo inasifiwa kwa kutenguwa matokeo ya Uraisi, wanasema ni ya kwanza Afrika na ya pili Duniani, wow, sifa kubwa.

Lkn kwa nini wameshindwa kuona kitu rahisi kama hiki kwenye Sensa yao? Nilikuwa Kenya juzi kati sasa hivi huko wanajadili Sensa ya watu, ni ugomvi kila mtu anaikataa, kila kundi linasema limehujumiwa kwa kupunguzwa ,,kwa makusudi” idadi yake.

Sasa swali langu, kwa nini Kenya wanauliza Kabila la mtu kwenye Sensa? Unataka kujua ili iwe nini? Nijuavyo TZ hairuhusiwi kuhesabu Makabila au hata Dini kwenye Sensa, kuna sababu kwa nini Waasisi wetu waliamua hivyo, nataka kujua mimi kama Serikali idadi ya Watoto, Wanawake, Wanaume, Walemavu na Wazee inayoishi sehemu fulani, sasa Kabila la nini?

Sasa Kenya ni shida, kila Kabila linataka kuwa na idadi kubwa, sijui ni kwa nini kwenye Katiba yao mpya, pendwa na bora kabisa Duniani walishindwa kuliona hili?
 
Wanaulizana makabila ili washindane kabila gani lina wanawake wazuri. Kabila la MK254 linaongoza kwa kuwa na wanawake wabaya, wavivu. Wanaofelifeli tu shuleni
 
Kwanza kabisa shukrani kwa kutambua na kukiri kwamba demokrasia yetu ni bora duniani, najua umetumia nguvu nyingi sana hadi kufikia kuukubali huo ukweli.

Pili, hili la makabila haitakua mara yangu ya kwanza kukujibu, unafaa ufahamu ukabila hauji kisa idadi imefahamika ya watu ndani ya makabila yao. Ubaguzi wa kikabila au ubaguzi mwingine wowote ni tabia ya mtu binafsi na mara nyingi husababishwa au kuchochewa na wanasiasa, ni kama kwa leo ilivyo huko Tanzania, watu wa upinzani wanabaguliwa kuliko wakati mwingine wowote kwenye historia ya nchi yenu, yaani huko kwenu leo hii kuitwa mpinzani imekua kama laana fulani, bila kusahau unyama wenu dhidi ya albino.

Nikirudi kwenye swali lako, sensa ni muhimu sana na hufanywa kisayansi ili kubaini mambo mengi sana, kila swali linaloulizwa humo lina sababu zake kisayansi, na hulikwepi kisa unaogopa mara ukabila, mara udini, utakua kama mbuni ambaye huficha kichwa na kuacha mwili wote uliwe shaba. Makelele ya baadhi ya wanasiasa hayafai ubadilishe masuala ya kisayansi, maana wao wana hulka ya kuhoji kila kitu, hata katiba yetu mpya ambayo ndio bora Afrika, wapo wanasiasa walioikataa na kudai kwamba itaruhusu ushoga, lakini leo hii kila mmoja ananufaika pakubwa.

Sisi kwetu Kenya hatupo radhi kufuta makabila yetu, maana ndio fahari yetu, tunasheherekea, kukumbatia na kuchangamkia tofauti zetu za mila na desturi tulizo nazo na kuukubali ukweli kwamba Mungu alikua na sababu zake za kutuumba watu kila mmoja na lugha yake ya asili, lakini pia tunafurahia utaifa wetu unaotuunganisha kama watu wa nchi moja.
 
OK, basi labda ni ,,culture clash” tu kama Wakenya wenyewe wanaona hamna tatizo na hilo basi labda ni mimi tu, kwani kwangu sikuona mantiki yoyote au uhusiano wowote wa Sensa ya Wakenya na idadi ya watu kwa kila kabila, lkn nimeelewa kwenu ina maana labda na manufaa pia.
 
Halafu nahisi ni kama una unafiki fulani kama ilivyo kawaida yenu, maana kwenu huko hoteli zote na magesti kwenye fomu lazima ujaze kabila lako, hicho hakipo huku.
Halafu kuna hii fomu yenu nimeiona kwenye mtandao inahoji kabila na dini

fomu.jpg
 
View attachment 1260437

Lkn hapa naongelea Sensa ya nchi iliyofanyika huko Kenya hivi karibuni.
 
Msijifanye malaika hats Tanzania idadi ya Kila kabila inajulikana.
Mwalium Nyerere RIP, alisema "Unataka kujua kabila la mtu ili iweje? Unataka kuandaa matambiko? Kama ni idadi ya wakristu au waislamu basi watajihesabu wenyewe huko makanisani na misikitini".
 
Kwanza kabisa shukrani kwa kutambua na kukiri kwamba demokrasia yetu ni bora duniani, najua umetumia nguvu nyingi sana hadi kufikia kuukubali huo ukweli.

Pili, hili la makabila haitakua mara yangu ya kwanza kukujibu, unafaa ufahamu ukabila hauji kisa idadi imefahamika ya watu ndani ya makabila yao. Ubaguzi wa kikabila au ubaguzi mwingine wowote ni tabia ya mtu binafsi na mara nyingi husababishwa au kuchochewa na wanasiasa, ni kama kwa leo ilivyo huko Tanzania, watu wa upinzani wanabaguliwa kuliko wakati mwingine wowote kwenye historia ya nchi yenu, yaani huko kwenu leo hii kuitwa mpinzani imekua kama laana fulani, bila kusahau unyama wenu dhidi ya albino.

Nikirudi kwenye swali lako, sensa ni muhimu sana na hufanywa kisayansi ili kubaini mambo mengi sana, kila swali linaloulizwa humo lina sababu zake kisayansi, na hulikwepi kisa unaogopa mara ukabila, mara udini, utakua kama mbuni ambaye huficha kichwa na kuacha mwili wote uliwe shaba. Makelele ya baadhi ya wanasiasa hayafai ubadilishe masuala ya kisayansi, maana wao wana hulka ya kuhoji kila kitu, hata katiba yetu mpya ambayo ndio bora Afrika, wapo wanasiasa walioikataa na kudai kwamba itaruhusu ushoga, lakini leo hii kila mmoja ananufaika pakubwa.

Sisi kwetu Kenya hatupo radhi kufuta makabila yetu, maana ndio fahari yetu, tunasheherekea, kukumbatia na kuchangamkia tofauti zetu za mila na desturi tulizo nazo na kuukubali ukweli kwamba Mungu alikua na sababu zake za kutuumba watu kila mmoja na lugha yake ya asili, lakini pia tunafurahia utaifa wetu unaotuunganisha kama watu wa nchi moja.
Kwa kiswahili hiki ulichoandika wewe sio mkenya au umetokea kenya ya pwani, wakenya wa kibara hawajui kiswahili kwa sampuli hii
 
Wewe nawe mnafiki. Ungekuwa unajivunia Ukikuyu usingemuoa Mluhya. Umepotea njia, watoto wako hawawezi kuwa Wakikuyu tena.
 
Halafu nahisi ni kama una unafiki fulani kama ilivyo kawaida yenu, maana kwenu huko hoteli zote na magesti kwenye fomu lazima ujaze kabila lako, hicho hakipo huku.
Halafu kuna hii fomu yenu nimeiona kwenye mtandao inahoji kabila na dini

View attachment 1260437
Hoteli zote na guest houses? Uongo mtakatifi huo. Mtu mzima unadanganya ili ushinde tu point, ujinga huo.
 
Kwanza kabisa shukrani kwa kutambua na kukiri kwamba demokrasia yetu ni bora duniani, najua umetumia nguvu nyingi sana hadi kufikia kuukubali huo ukweli.

Pili, hili la makabila haitakua mara yangu ya kwanza kukujibu, unafaa ufahamu ukabila hauji kisa idadi imefahamika ya watu ndani ya makabila yao. Ubaguzi wa kikabila au ubaguzi mwingine wowote ni tabia ya mtu binafsi na mara nyingi husababishwa au kuchochewa na wanasiasa, ni kama kwa leo ilivyo huko Tanzania, watu wa upinzani wanabaguliwa kuliko wakati mwingine wowote kwenye historia ya nchi yenu, yaani huko kwenu leo hii kuitwa mpinzani imekua kama laana fulani, bila kusahau unyama wenu dhidi ya albino.

Nikirudi kwenye swali lako, sensa ni muhimu sana na hufanywa kisayansi ili kubaini mambo mengi sana, kila swali linaloulizwa humo lina sababu zake kisayansi, na hulikwepi kisa unaogopa mara ukabila, mara udini, utakua kama mbuni ambaye huficha kichwa na kuacha mwili wote uliwe shaba. Makelele ya baadhi ya wanasiasa hayafai ubadilishe masuala ya kisayansi, maana wao wana hulka ya kuhoji kila kitu, hata katiba yetu mpya ambayo ndio bora Afrika, wapo wanasiasa walioikataa na kudai kwamba itaruhusu ushoga, lakini leo hii kila mmoja ananufaika pakubwa.

Sisi kwetu Kenya hatupo radhi kufuta makabila yetu, maana ndio fahari yetu, tunasheherekea, kukumbatia na kuchangamkia tofauti zetu za mila na desturi tulizo nazo na kuukubali ukweli kwamba Mungu alikua na sababu zake za kutuumba watu kila mmoja na lugha yake ya asili, lakini pia tunafurahia utaifa wetu unaotuunganisha kama watu wa nchi moja.

Mleta mada utakua umepata muongozo...

Cc: mahondaw
 
Wewe nawe mnafiki. Ungekuwa unajivunia Ukikuyu usingemuoa Mluhya. Umepotea njia, watoto wako hawawezi kuwa Wakikuyu tena.

Mada kama hizi za kutaja makabila huwa kama asali kwako, chunga usije kuachia ukabila ukakumaliza.
Mimi najivunia Ukikuyu maana ndio asili yangu, sikuzaliwa Mkikuyu kwa bahati mbaya, ndiko walikozikwa mababu zangu, na kila nikienda kuwasabahi watu wetu kule huwa natiririka Kikikuyu hadi raha.
Lakini pia hata hapa mjini huwa natumia lugha yangu ya asili sehemu stahiki, ukizingatia pia nimejifunza lugha kadhaa za huku kwetu.

Kila mmoja wetu dunia hii ana asili yake, hata ukizamia kwa Wazaramo Dar na kujifanya Mswahili, ukweli ni kwamba hutafuta asili ya ulikotoka, kwa njia moja au nyingine kuna kitu ndani yako kimeunganika na mababu zako. Watanzania mnaishi vibaya sana kwa kukana na kutelekeza asili zenu.

Hata hivyo, Mzungu alikuja akachora chora mipaka na kuwakusanya watu wa asili mbali mbali na kuwasindika kwenye makundi, kila kikundi akakipa taifa, na kuwaamrisha Waafrika waanze kuonana kwa misingi ya hayo makundi, hivyo mababu zangu wakajipata ndani ya kikundi cha Kenya, nimezaliwa na kuikuta hali ikiwa hivyo, nikaikumbatia na kujivunia Ukenya japo bila kusahau asili yangu ya Ukikuyu.
Zaidi ya hapo, nasheherekea Uafrika unaotuleta pamoja kwenye bara hili licha ya kutenganishwa na michoro ya mkoloni, hamna kitu huniuma kama ninapotembelea mojawapo wa haya mataifa halafu uhamiaji wananihoji siku ninazokusudia kukaa humo. Yaani mtaani unapishana na watu mnaofanana katika kila hali, mnaotaniana kama ndugu, ila siku zako zinajihesabu na zikiisha lazima uondoke.
Ndio yale ya Afrika Kusini, Waafrika weusi wanatembezana mapanga kwa misingi ya hiyo michoro iliyowekwa na mzungu.
 
Kwanza kabisa shukrani kwa kutambua na kukiri kwamba demokrasia yetu ni bora duniani, najua umetumia nguvu nyingi sana hadi kufikia kuukubali huo ukweli.

Pili, hili la makabila haitakua mara yangu ya kwanza kukujibu, unafaa ufahamu ukabila hauji kisa idadi imefahamika ya watu ndani ya makabila yao. Ubaguzi wa kikabila au ubaguzi mwingine wowote ni tabia ya mtu binafsi na mara nyingi husababishwa au kuchochewa na wanasiasa, ni kama kwa leo ilivyo huko Tanzania, watu wa upinzani wanabaguliwa kuliko wakati mwingine wowote kwenye historia ya nchi yenu, yaani huko kwenu leo hii kuitwa mpinzani imekua kama laana fulani, bila kusahau unyama wenu dhidi ya albino.

Nikirudi kwenye swali lako, sensa ni muhimu sana na hufanywa kisayansi ili kubaini mambo mengi sana, kila swali linaloulizwa humo lina sababu zake kisayansi, na hulikwepi kisa unaogopa mara ukabila, mara udini, utakua kama mbuni ambaye huficha kichwa na kuacha mwili wote uliwe shaba. Makelele ya baadhi ya wanasiasa hayafai ubadilishe masuala ya kisayansi, maana wao wana hulka ya kuhoji kila kitu, hata katiba yetu mpya ambayo ndio bora Afrika, wapo wanasiasa walioikataa na kudai kwamba itaruhusu ushoga, lakini leo hii kila mmoja ananufaika pakubwa.

Sisi kwetu Kenya hatupo radhi kufuta makabila yetu, maana ndio fahari yetu, tunasheherekea, kukumbatia na kuchangamkia tofauti zetu za mila na desturi tulizo nazo na kuukubali ukweli kwamba Mungu alikua na sababu zake za kutuumba watu kila mmoja na lugha yake ya asili, lakini pia tunafurahia utaifa wetu unaotuunganisha kama watu wa nchi moja.
Kuwa Tanzania haimaanishi kuwa hatutambui kinachoendelea katika siasa za Kenya, kwa hiyo wanapo taja Deomokrasia ya Kenya kuwa juu,huwa sisi tunajiuliza KIVIPI ?
iwapo mtatupa majibu kivipi demokrasia yeniu ni bora,sisi tutawapa majibu ni vipi demokrasia yenu ni bandia katika Afrika.
Ila sishangai sana,maana kila mkenya anaekuja Tanzania anatokea Nairobi,hivi huko hamna miji mingine ?
Natania tu.
 
Mleta uzi ni Mtanzania mwenzio na alitanguliza kwa kusifia demokrasia yetu.....
 
Pamoja na demokrasia yao nzuri na bora kabisa Duniani ambayo inasifiwa kwa kutenguwa matokeo ya Uraisi, wanasema ni ya kwanza Afrika na ya pili Duniani, wow, sifa kubwa.

Lkn kwa nini wameshindwa kuona kitu rahisi kama hiki kwenye Sensa yao? Nilikuwa Kenya juzi kati sasa hivi huko wanajadili Sensa ya watu, ni ugomvi kila mtu anaikataa, kila kundi linasema limehujumiwa kwa kupunguzwa ,,kwa makusudi” idadi yake.

Sasa swali langu, kwa nini Kenya wanauliza Kabila la mtu kwenye Sensa? Unataka kujua ili iwe nini? Nijuavyo TZ hairuhusiwi kuhesabu Makabila au hata Dini kwenye Sensa, kuna sababu kwa nini Waasisi wetu waliamua hivyo, nataka kujua mimi kama Serikali idadi ya Watoto, Wanawake, Wanaume, Walemavu na Wazee inayoishi sehemu fulani, sasa Kabila la nini?

Sasa Kenya ni shida, kila Kabila linataka kuwa na idadi kubwa, sijui ni kwa nini kwenye Katiba yao mpya, pendwa na bora kabisa Duniani walishindwa kuliona hili?
Wewe km ni msukuma kamwe haiwezi badilika..hata ukajisifia kiswahili bado kwako itabaki lugha ya kuja tu
 
Kujadiliana na Wakenya humu unahitaji uvumilivu sana, wana vichwa vigumu kama mawe

Sasa kuhesabiwa kimakabila nchini na kujaza taarifa binafsi kwenye fomu individually wapi na wapi
Kuhesabu kikabila au kusema kabila lako unapoingia gesti..gani ya kiboya
 
Wewe km ni msukuma kamwe haiwezi badilika..hata ukajisifia kiswahili bado kwako itabaki lugha ya kuja tu

Ina uhusiano gani na Mada husika? Isitoshe mimi siyo Msukuma, asili yangu ni Rufiji kama ulipenda kujua.
 
Back
Top Bottom