Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,817
Pamoja na demokrasia yao nzuri na bora kabisa Duniani ambayo inasifiwa kwa kutenguwa matokeo ya Uraisi, wanasema ni ya kwanza Afrika na ya pili Duniani, wow, sifa kubwa.
Lkn kwa nini wameshindwa kuona kitu rahisi kama hiki kwenye Sensa yao? Nilikuwa Kenya juzi kati sasa hivi huko wanajadili Sensa ya watu, ni ugomvi kila mtu anaikataa, kila kundi linasema limehujumiwa kwa kupunguzwa ,,kwa makusudi” idadi yake.
Sasa swali langu, kwa nini Kenya wanauliza Kabila la mtu kwenye Sensa? Unataka kujua ili iwe nini? Nijuavyo TZ hairuhusiwi kuhesabu Makabila au hata Dini kwenye Sensa, kuna sababu kwa nini Waasisi wetu waliamua hivyo, nataka kujua mimi kama Serikali idadi ya Watoto, Wanawake, Wanaume, Walemavu na Wazee inayoishi sehemu fulani, sasa Kabila la nini?
Sasa Kenya ni shida, kila Kabila linataka kuwa na idadi kubwa, sijui ni kwa nini kwenye Katiba yao mpya, pendwa na bora kabisa Duniani walishindwa kuliona hili?