Simba zee 33
JF-Expert Member
- Sep 15, 2020
- 1,374
- 1,564
Wakati Jakaya anamalizia malizia uongozi wake alipata fursa ya kuhutubia bunge la kenya na akasema.Acheni uongo, wakenya hawana uhasama wowote na TZ, kilichopo ni utani wa kawaida tu kati ya raia wa Kenya na TZ ambao upo kwa mataifa mengi tu duniani.
The only minor exception ni kwamba utawala wa JPM umeongeza changamoto kadhaa kwenye mahusiano yetu na Kenya. Kwa mfano, Kulikuwa na haja gani kuchoma vifaranga hai kutoka Kenya tena katika hali ya uwazi na majigambo vile? Vilevile, badala ya kutumia diplomacy kutatua tofauti zetu na Kenya, sisi tuko busy na tit-for-tat foreign policy.
Acha niwape mfano mmoja wa nini maana ya diplomacy. Chukulia mfano UK ilivyojitoa umoja wa ulaya (EU). Usidhani kwamba Germany, France, na nchi zingine za Ulaya hawajui nini kilikuwa nyuma ya ule mpango dhalimu wa Uingereza kujitoa umoja wa Ulaya. Ikumbukwe kwamba, EU wana mkakati wa muda mrefu wa kupunguza mafungamano yake na Marekani kiuchumi, kisiasa, kiteknolojia na kiusalama. Several attempts za kudhoofisha nguvu hii ya EU zishafanyika lakini zote zimeshindwa kuidhoofisha EU, all to the detriment of US interest in Europe. Hata mafungamano ya kiuchumi kati EU na Russia yalikuwa yameshaanza kupanda kwa kasi, but akatengeneza mgogoro wa Ukraine( through color revolution) ili kuhakikisha EU na Russia hazishirikiani kiuchumi. Kwahiyo Uingereza, alitumika na USA kama chambo ili kujitoa kwake EU kutengeneze spiral effect ya kuidhoofisha EU. Wababe wa EU yaani Germany na France wanaujua mchezo wote, lakini angalia wanavyoijadili EXIT PACKAGE ya UK kwa diplomacy ya upole na ustaarabu bila kuleta taharuki yoyote. Na tayari UK kashapewa na uso na EU coz unafuu aliokuwa unautafuta katika kufanya biashara na EU amenyimwa.
TZ ina tatizo kubwa sana kwenye diplomasia ya kimataifa, hasa kipindi hiki. Hiki ndio kilema chetu watanzania kwa sasa, na hakuna uhasama wowote na Kenya zaidi ya political skirmishes.
"Mimi naondoka madarakani nikiacha nchi yetu Ikiwa na uhusiano mzuri sana na Kenya kuliko wakati wowote.. Mimi nawahakikishieni ndugu zangu Wakenya uhusiano wetu utaendelea kua mzuri labda atokee mtu mjinga mpumbavu na waajabu sana,, na watu wa Aina hio ni wachache sana kwetu Tanzania '' mwisho wa kunukuu.
Wachambuzi wa Mambo wanasema Mtu mjinga, mpumbavu na waajabu sana ni mmoja tu hapa Tanzania na wala sio wachache kama mzee kikwete alivyodai.