Huyu bwana kwa taaluma yake na kwa jinsi anavyojipambanua kama mwanasheria nguli, nilitaraji niwe nimemuona katika viunga vya mahakama mara kadhaa. Sababu kubwa ni kwa kujua na Lissu anajua sana, kuwa kwa mujibu wa Katiba yetu, mahakama ndio mhimili uliopewa mamlaka ya kusimamia na kutoa haki katika Nchi.
Lissu anadai kupitia katika matukio mazito, ambayo kisheria, yalipaswa kuwa yamefika Mahakamani ili sio tu kulinda na kutetea Haki yake Lakini pia kuweka msingi kwa haki za wengine.
1) Lissu alinusurika kuuawa na kupigwa risasi nyingi tu. Na alisema waliotaka kumuua anawafahamu. Aliwahi kukaririwa akisema "I have survived to tell a tale". Kilichotokea Hadi Leo ni kurusha tu tuhuma na lawama hadharani kwenye mikutano na vikao bila hatua yeyote ya kisheria
2) Lissu kaja na tuhuma za kuhongwa mamilioni na mtoto wa Rais bila shaka Ili ahujumu chama chake. Kuhongwa/Rushwa ni Kosa kubwa kisheria. Hapa napo hajaweza kuchukua hatua zozote za kisheria zaidi kumwaga tuhuma hizo hadharani Kila siku.
3) Lissu amedai na anadai kutishwa na amepokea Taarifa za kuaminika za kuuawa. The same story, hakuna hatua anazoonekana kuchukua zaidi ya maneno anayotamka hadharani.
Najiuliza ni hofu gani huwa anaipata Lissu ku initiate hatua za kisheria dhidi ya madhila haya anayodai kumpata ambayo pia ni kinyume kabisa na Sheria za Nchi? Kama mambo mazito kama haya yanashindikana kwa Lissu, vipi kwa Mtanzania wa kawaida?